December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UWT Mkoa yawapiga msasa Makatibu Kimanga

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Umoja wanawake UWT mko a Dar es Salaam imewataka Makatibu wa UWT ngazi ya Kata na Matawi kufanya kazi za Jumuiya na kufanya vikao vya UWT Sambamba na Kusoma Kanuni.

Hayo yalisemwa na Katibu wa Mkoa Dar es Salaam wa Umoja wanawake UWT Asha Stambuli wakati wa Ziara yake na Kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa Jimbo la segerea.

“Nawaomba Makatibu kata na ngazi ya matawi kufanya kazi za jumuiya,kufanya vikao pamoja na kusoma kanuni kwa ajili ya kuongoza Jumuiya yenu vizuri”alisema Asha.

Katibu Asha alisema ili Jumuiya iweze kusonga mbele ni lazima viongozi wake wafanye kazi na kufuata Kanuni ya Jumuiya inavyoelekeza mambo mbali mbali ikiwemo kufanya vikao .

Aidha alisema pia ili Jumuiya iweze kusonga mbele lazima iwe na mtaji wa Wanachama wengi hivyo aliwataka kila kiongozi wa Kamati ya Utekelezaji kuleta wanachama wapya na kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za ELECTONIC.

Wakati huo huo aliwataka UWT Jimbo la segerea na Kimanga viongozi waliochaguliwa na kushindwa kushiriki vikao na kufanya kazi waondolewe wachaguliwe Wengine kuziba nafasi zilizopo wazi.

Katika hatua nyingine Katibu wa Mkoa wa UWT aliwamasisha wanawake kuchukua fomu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ajili ya kugombea mwaka huu 2024.

Pia alihamasisha Kushiriki kujiandikisha katika Daftari la Makazi na Daftari la mpiga kura waweze kupata haki ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa .

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Ilala Mariam Bakari alisema dhumuni la ziara ya UWT mkoa kuangalia uhai wa jumuiya na uingizaji wanachama ngazi ya matawi ambapo pia aliwataka UWT Kimanga kuongeza wanachama wapya na kufanya vikao kila mwezi.

Mwenyekiti wa UWT Kimanga Dkt.Marysia Tukai alisema katika ziara hiyo UWT Kimanga wamejifunza mambo mengi na wamepata chakula ya ubongo watafanya mambo makubwa imekuwa chachu ya kuongeza kufanya kazi kwa weledi katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ikiwemo kuongeza wanachama wapya na kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za ELECTONIC.

Katibu wa UWT kata ya Kimanga Amina Msago akimkabidhi zawadi Maalum Katibu wa UWT Wilaya ya Ilala Mariam Bakari Katika Ziara ya UWT Mkoa Dar Es Salaam leo Juni 04/2024 zawadi hiyo imetolewa na Uongozi wa Umoja Wanawake Kata ya KIMANGA ,Ziara hiyo Dhumuni lake kuangalia uhai wa Jumuiya (Katikati)anayeshudia Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kimanga Dkt.Marysia Tukai (PICHA NA HERI SHAABAN)
Katibu wa umoja wanawake UWT kata ya Kimanga Amna Msago akimkabidhi zawadi Maalum Katibu wa UWT Mkoa Dar Es Salaam Asha Stambuli leo Juni 04/2024 zawadi hiyo Imetolewa na Uongozi wa UWT Kata ya Kimanga (Katikati )Mwenyekiti wa UWT kata ya Kimanga Dkt.Marysia Tukai (PICHA NA HERI SHAABAN)