Na Heri Shaaban (Ilala)
Jumuiya ya Wanawake UWT Wilaya ya Ilala imewataka viongozi wa jumuiya hiyo ambao wamechaguliwa wanashindwa kutekeleza Majukumu yao wakae pembeni wachaguliwe wengine .
Mwenyekiti wa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa alisema hayo Kata ya BONYOKWA wilayani Ilala Katika ziara ya Kamati ya utekelezaji Uwt kuwashukuru Wanachama .
“Ninaagiza kuanzia ngazi ya matawi na ngazi ya Kata kama kuna viongozi wamechaguliwa wanashindwa kutekeleza Majukumu yao Sasa wakae pembeni wachaguliwe wapya watakaoweza kufanya kazi za jumuiya na kazi za chama “alisema Neema .
Mwenyekiti Neema alisikitishwa kupewa Taarifa Kata ya BONYOKWA uhai wa JUMUIYA hiyo ya UWT umelala Wakati kuna Jeshi kubwa la Wanawake ndani ya Kata hiyo .
Aliagiza Kata ya BONYOKWA na Kata zingine ambazo viongozi wa matawi na Kata wameshindwa kusimamia Majukumu yao wakae pembeni waweze kuchaguliwa Wanawake wapya wa UWT watakao weza kuongoza jumuiya hiyo vizzuri .
Aliwataka Wanawake wa UWT kuwa wamoja kudhidisha upendo kushirikiana na chama na Serikali Katika utekelezaji wa majukumu yao .
Alisema wale wenye mapenzi mema na chama wamejitoa Kwa mapenzi Yao wamegombea uongozi wafanye kazi waweze kukipigania chama kiweze kushika Dola Katika chaguzi wa Serikali za Mitaa wajitokeze Kwa wingi kuchukua fomu za Uongozi .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Neema Kiusa alitoa agizo akitaka viongozi wa BONYOKWA wa UWT ndani ya Mwezi Mmoja waangize wanachama wapya 500.
Wakati huohuo Mwenyekiti Neema aliwataka wanawake kulea Watoto wao katika Mazingira Bora kama mboni ya jicho lao waache kutumia nguvu katika Malezi ya watoto .
Kaimu Katibu wa Umoja wanawake Wilaya ya Ilala Mariamu Bakari aliwataka wamashishe kuingiza wanachama wapya waweze kuwasajili katika mfumo wa electronic walipe na ada ya uwanachama Kila mwaka.
Aidha Mariamu Bakari aliwataka UWT waunde Kamati za Wajumbe wa Mashina Kwa ajili ya kusaidiana na Jumuiya hiyo kufanya kazi za UWT .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi