November 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UWT Ilala yapiga marufuku wageni kulala na watoto chumba kimoja

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, llala

Umoja wa Wanawake (UWT )Wilaya ya Ilala imepiga marufuku wageni kulala chumba kimoja na watoto na kuwataka wazazi kuchukua hatua katika kuwalinda watoto wao na kukomesha vitendo vya ukatili .

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa alitoa tamko hilo kata ya GONGOLAMBOTO wakati wa kufungua baraza la Uwt kata hiyo baraza lililouzuliwa na Madiwani wa Viti Maalum ,Julieth Banigwa ,Semeni Mtoka na Eva Nyamoyo .

“Wanawake wenzangu wa Wilaya ya Ilala Naomba tushirikiane katika kukemea vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika katika majumba yetu tuchukue hatua mbalimbali za kuwalinda watoto Wetu wasilale na wageni chumba kimoja usimwamini mtu yoyote ” alisema Neema .

Mwenyekiti Neema alisema wazazi watakapokemea vitendo vya ukatili kila Mmoja hatakuwa mlinzi wa mwezake katika kulinda Jamii na vizazi vijavyo .

Wakati huo huo Mwenyekiti Neema aliwataka Wanawake kushirikiana pamoja kujenga chama na Jumuiya kwa sasa kadi zipo za kutosha hivyo wafike wilayani kuchukua kadi na kuongeza wanachama wapya kwa ajili ya uhai wa Jumuiya na kata itakayofanya vizuri itapewa Zawadi nono kwa ajili ya kuongeza wanachama .

Aidha alisema bila chama amna UWT aliwataka Shughuli zozote za UWT wapewe baraka na CCM

Aliwataka Wanawake wafanye kazi za chama na nje ya chama katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasaan Ikiwemo wafanye ziara kutembelea makundi maalum ya mitaani kwa sasa wasilale wakati wa kusaka Dola umefika .

Diwani wa Viti Maalum Julieth Banigwa aliwapongeza Viongozi waliochaguliwa waweze kukisemea chama kwani wao ni dhamana madiwani wa Viti Maalum wapo Pamoja nao katika kuwasaidia .

Diwani Semeni Mtoka alisema Kata ya Gongolamboto Kata inayoongoza kuwa na miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo madaraja makubwa mawili,shule ya kisasa English Medium na kituo cha Afya .

Diwani Semeni Mtoka aliwataka washirikiane na Diwani wao Lucas Lutainurwa katika kuleta MAENDELEO CCM isonge mbele

Aliwataka watafute Viongozi wenye mapenzi mema na chama cha Mapinduzi kama Diwani Lucas ambaye anasimama imara kuwatetea wananchi wao Gongolamboto iweze kupata Maendeleo .

Katibu wa UWT Kata ya Gongolamboto akikabidhi risala Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa wakati wa kufungua Baraza la UWT Gongolamboto Leo February 12/2023 (Katikati)Mwenyekiti wa UWT Gongolamboto Yasinta Mutayabarwa.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya llala Neema Kiusa akizungumza na Wanawake wa UWT Kata ya GONGOLAMBOTO hawapo (Pichani) Leo February 12/2023 wakati wa kuzindua baraza la uwt Kata GONGOLAMBOTO.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ilala Neema Kiusa (Kulia wa kwanza )(katikati Mwenyekiti wa UWT Gongolamboto Yasinta Mutayabarwa na Katibu wa uwt Gongolamboto sijali Ally wakiwa katika Baraza la uwt Gongolamboto