November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UWT Ilala watoa tuzo kwa Mwenyekiti Said

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala imetoa tuzo kwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Ilala Said Sidde kwa kufanya kazi za chama kwa weledi huku akiwa Mlezi wa Jumuiya hiyo UWT.Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa ,alitoa tuzo hiyo kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala katika kikao cha Baraza la UWT ukumbi wa Mikutano Arnatogluo Wilayani Ilala .

“UWT Wilaya ya Ilala na Kamati yetu ya Utekekezaji tumetoa tuzo iliyotukuka kwa Mwenyekiti wetu Said Sidde, kwa ushirikiano anaotupa Jumuiya yetu ya wanawake Wilaya ya Ilala na kusimamia chama vizuri amekuwa Mwenyekiti wa çcm wa Wilaya wa mfano muda wote kazi tuu ” alisema Neema .

Mwenyekiti Neema alisema UWT Wilaya ya Ilala ipo imara kwa kushirikiana na chama cha Mapinduzi CCM ambapo mpaka sasa UWT Wilaya imevuna jumla ya wanachama wapya 6000 .

Neema aliwataka wanawake wa UWT Wilaya ya Ilala wawe na upendo na mshikamano wenyewe kwa wenyewe , Jumuiya na ndani ya chama.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Neema Kiusa, aliwataka Madiwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama kabla mwezi Julai kumalizika .

Aidha aliwataka wanawake wa UWT wafanye kazi kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi ,chama na Serikali .Mwenyekiti wa Çhama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde hotuba yake leo ilikuwa inalenga vifungu vya kanuni za Umoja na Wanawake ,na kufuata madhumuni ya UWT ambayo yote yapo katika kanuni za UWT.

Mwenyekiti Sidde pia aliwaasa Wanawake wapendane washirikiane wasijirudishe nyuma katika kugombea nafasi kubwa za chama ,na Serikali Ili waje saidia Wananchi wawe kioo cha Jamii Aliwataka wampe ushirikiano Mwenyekiti wa UWT Neema Kiusa na Kaimu Katibu wake Mariam Bakari .

Katika Baraza la Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Madiwani watatu wa Viti Maalum walifanikiwa kuwashirisha Taarifa za Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi Cha miezi sita madiwani hao Moza Mwano ,Semeni Mtoka ,Beatrice Edward.