Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala imeshiriki mapokezi ya Mwenge wa UHURU mwaka 2024 katika mapokezi hayo Mwenyekiti wa Umoja wanawake Wilaya ya Ilala NEEMA KIUSA aliongoza Wanawake wa UWT wa wilaya ya Ilala.
Mwenyekiti NEEMA KIUSA alisema wanaipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM vizuri ambapo leo miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu inazinduliwa na Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava .
Mwenyekiti NEEMA alipongeza Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Madiwani wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo Mkurugenzi wa jiji Jamary Mrisho Satura kwa usimamizi mzuri wa mapato katika wilaya ya Ilala na kufanikiwa kujenga miradi mikubwa ya maendeleo.
“UWT tunaunga mkono juhudi za Serikali leo tumeshiriki mapokezi ya Mwenge wa UHURU Pamoja na Kamati yangu yote ya Utekelezaji mabaraza ya UWT kwa ajili ya kushiriki shughuli za Serikali “alisema Neema.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â