Na David John, Geita
MAABARA inayopima sampuli za Madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa (MSALABS) imewekeza zaidi ya shilingi bilioni tano za kitanzania katika Mkoa wa Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara hiyo Mugisha Lwekoramu ameyasema hayo wakati wa uwekeaji jiwe la msingi la ofisi hiyo iliyojengwa katika halmashauri ya mji wa Geita na kutarajiwa kuanza kazi rasmi ya upimaji wa samapuli hizo Noevemba mwaka huu.
Amesema,maabara hiyo yenye Makao yake Makuu nchini Canada inafanaya kazi kwa viwango vya kimataifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa mionzi yaani (PhotoAssay) ambayo ni rafiki kwa utunzaji mazingira kwasababu haitumii kemikali au moto katika upimaji sampuli.
Lwekoramu ameeleze ufanisi wa teknolojia hiyo ambapo amesema hii ni sehemu ya mapinduzi ya teknolojia kwasababu inamwezesha mdau kupata majibu ya sampuli ndani ya masaa mawili ni tofauti ukilinganisha na teknolojia ya zamani ya kutumia moto na kemikali.
Kwa upande Waziri wa Madini Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini , akiwataka kuendelea kufungua matawi mengine nchini huku akiahidi kuwa Serikali Awamu ya Sita itaendelea kuwatengenezea mazigira rafiki ya uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa jinsi itakavyohitajika katika mnyororo mzima wa sekta madini.
Aidha, amewapongeza kwa kuweza kuajiri watanzania kwa asilimia 99.8 akiamini kuwa wafanyakazi hao wataendelea kujifunza utumiaji wa teknolojia hiyo na kutoa ujuzi huo kwa watanzania wengine.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amesema,uwekezaji huo ni kutokana na uwepo wa Rais Makini anayesimamia vyema na kuweka mzingira mazuri ya uwekezaji kwa lengo la kuvutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais