Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
UMOJA wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa leo wamezindua kampeni ya kuhamamsisha watu kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ikiwa ni jitihada za kuunga mkono serikali katika kuhakikisha watu wanajitokeza na kuhesabiwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Kitika viwanja vya mwembeyanga Jijini Dar es salaam katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Kenani Kihongosi amesema sensa ni msingi wa maendeleo ya nchi na inabeba dhana nzima ya ajenda ya maendeleo hivyo vijana wanapaswa kushiriki kwa kujitolea kuhamasisha jamii yote iweze kishiriki.
“Wajibu wetu ni kuhakikisha tunaungana na serikali na kuwaeleza watanzania na vijana wenzetu kwamba sensa ni kitu muhimu na tunaisaidia serikali katika kuisukuma agenda ya maendeleo” amesema Kihongosi
Kihongosi ameongeza kuwa kampeni hiyo imezinduliwa Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Juni 23, 2022 lakini litakua endelevu katika Mikoa mingine kwa hamasa kubwa kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu na Serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza ilani ya CCM kuhakikisha Serikali inatambua watu wake ili kupeleka maendeleo kulingana idadi.
Kihongosi amesema kuwa kampeni hiyo itaambatana na wataalamu mbalimbali wa sensa kutoka serikalini ambao watatoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa sensa na faida zake na zaidi kuwajulisha watu umuhimu wa kutambulika na serikali ili kupata taarifa za msingi zinazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025,mageuzi ya masula ya afya na jamii,na ajenda za ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo kimataifa.
Kwa upande wake katibu UVCCM mkoa wa Dar es salaam Mussa Kilakala amesema watahakikisha elimu ya sensa inamfikia kila mwanaDar es salaam kwani taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.
‘Umoja wa vijana Taifa umeona kwa umuhimu wa tukio hili kwa kutambua fursa za maendeleo zilizopo, Kw kutambua taifa letu linatoka wapi na linataka kwenda wapi, limeona umuhimu wa kuhamasisha sensa hii kupitia vijana wenzetu” amesema Mussa
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba