Na Penina Malundo, timesmajira
Ufuatiliaji wa kanuni bora za afya,ufugaji wa mifugo pamoja na utunzaji wa mazingira ni miongoni mwa mambo ambayo yakizingatiwa yanaweza kupunguza janga la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.
Hali ya ugonjwa wa usugu wa vimelea vya magonjwa kwa sasa ni kubwa kidunia kutokana na jamii kutojua ugonjwa huo, ambapo umekuwa unatafuna watu bila kujijua kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa ugonjwa wa usugu wa Vimelea vya Magonjwa kitaalam unasababishwa na matumizi yasiyosahihi ya dawa pekee.
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kwamba ugonjwa huo ni moja ya matishio makuu 10 ya afya ya umma duniani yanayowakabili binadamu kwani ugonjwa huo licha ya kupatikana katika dawa pia inapatikana kwa wanyama pamoja na mazingira yanayowazunguka watu.
Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO )inakadiriwa kwamba watu 700000 hufa kila mwaka kutokana na maambukizi yanayotokana na hali ya usugu wa dawa ambapo ripoti ya mwaka 2019 ya Kikundi cha Umoja wa Mataifa kinachoratibiwa na mashirika ya WHO na FAO ilionyesha kwamba magonjwa yanayosababishwa na hali ya usugu wa dawa yanaweza kusababisha vifo vya watu milioni 10 kila mwaka kufikia 2050.
Hivyo kuna umuhimu wa kuelimisha watu kuhusu hatari za kutumia antibayotiki bila maelekezo yanayofaa kutoka kwa daktari aliyehitimu chuo iwe kwenye suala la afya,kilimo au mifugo ni vema kuhakikisha ushauri wao unafatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya wanahabari yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Media Foundation (TMF) kwa waandishi wa habari wa masuala ya afya,Mfamasia Josephat Hema amesema miaka ya 1944 kulikuwa hakuna ugonjwa huo kutokana na kutokuwa na dawa za kutibu vimelea hivyo .
Anasema baada ya watafiti na watafiti mbalimbali kugundua dawa hizo,zilianza kutumika vizuri na kusaidia magonjwa ila baada ya kuzoeleka na watu kuanza kutumia kiholela ndipo dawa hizo zilikosa nguvu ya kuua wadudu na kufanya kuwepo kwa usugu wa vimelea vya magonjwa.
Josephat anasema vidudu hivyo vya vimelea vya magonjwa vipo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo udogo,miti, mwili wa binadamu na mnyama ambapo wadudu hao wapo aina mbili wapo wanaosababisha magonjwa na wanaopambana na magonjwa.
”Utumiaji wa dawa za Auntibayotic kiholela inaenda tumboni inaua waudu wote wale wanasababisha magonjwa na wale wazuri wanaopambana na magongwa wanabaki na kuongezeka zaidi na kuwa wengi kisha kuanza kugeuka kuwa tatizo,”anasema na kuongeza
‘Unapotumia dawa kiholela tatizo la usugu wa dawa linakuwa kubwa na kusababisha kuenea, mwisho wa siku unajikuta kuwa ugonjwa unaoumwa hauponi,kitaalamu wadudu wanaokuwa wanausugu wa dawa wanauwezo wa kuambukiza wadudu wengine ambao tatizo linazidi kuwa kubwa,”anasema.
Akitaja sababu zinazofanya usugu wa vimelea vya magonjwa kusambaa ni pamoja na ukosefu wa dawa mpya wa kutibu magonjwa haya,matumizi ya dawa za antibiyotic kiholela,kutokuwa na tabia ya usafi ukiwa na kutofata kanuni ya usafi ikiwemo kutosafisha mikono au vyombo unavyotumia inasababisha kusambaza wadudu hao ambao ni sugu.
Aidha Josephat anasema pia kuna dawa za kutibu kuku au ng’ombe nazo ni changamoto kubwa kwani dawa hizo wanapowekewa wanayama hao na kuingia katika miili yao na mtu unapokuja kutumia kitoweo au nyama yao bila kusubiri kwa siku saba kama wataalamu wanavyoshauri inasababisha binadamu kupata usugu wa dawa kutokana na dawa walizokuwa nazo wanyama hao .
Pia anasema mbali na hiyo yapo maeneo ya hospitalini na nyumba za wazee watu wanaokuwa na magonjwa na endapo kama hakuna tabia ya kufanya usafi itapelekea wale wadudu wa usugu wa magonjea kuhamia kwa watu ambao hawana ugonjwa huo.
Anasema mwaka 2030 patakuwa na ongezeko la matumizi ya Antibiotic mfano kwa asilimia 67 hususan katika nchi ambazo uchumi wa chini na kati lakini pia katika nchi hizo uzalishaji utaweza kupungua kwa asilimia 10 kwa nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake Mhadhiri na Mshauri wa Chuo Kikuu Cha Afya na SAYANSI Shirikisho Muhimbiki (MUHAS)Dkt,Maurice Mbunde anasema kuwa usugu wa vimelea vya magonjwa unavyanzo vingi lakini unaweza ukatokana na mtu kutomaliza dozi aliyoandikiwa na daktari au utumiaji holela wa dawa .”leo anaumwa hiki anatumia kidogo au mtu haumwi lakini yupo katika mazingira ambayo anakuwa anabeba vitu aina fulani yaenye Antibiyotic na vinaingia ndani ya mwili wake. bila yeye mwenyewe kutojifaha,”anasema
Anasema kwa sasa vimeibuka katika mfumo wa vile vitu vinavyoingia katika mwili kwa kutumia dawa au vyakula tunavyokula ikiwemo ulaji wa Kuku ambaye ametoka kutum Antibayotic au kula nyama ya ng’ombe aliyetumia dawa hizo kwa sasahali hiyo inaonekana ni tatizo.
”Vyakula tunavyokula vinakuwa vimewekewa dawa wanyama wanaumwa wamewekewa sindano , sasa bahati mbaya sehemu ambayo wanatibiwa mifugo zile dawa zinafikika kwa binadamu nao wanatumia vitu mbalimbali kutojua kula nyama ya ng’ombe aliyetibiwa ,”anasema.
Amesema usugu wa vimelea vya magonjwa inamaanisha ni hali ya vimelea kushindwa kudhibitiwa na dawa zilizotengenezwa dhidi yake ambapo zipo
dawa ambazo zimeshatengenezwa na zimelengwa kudhibiti au kuua wadudu aina mbalimbali wanaweza kuwa bakteria au fangasi lakini inafika hatua ya ile dawa inapotolewa na kutumika kwa wanyama au binadamu badala ya wadudu kuisha au kuuawa wale wadudu ubaki kuwa hai.
***TMDA yasema juu ya usugu wa Dawa
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Adam Fimbo amesema wananchi na jamii wanapaswa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuepuka matumizi holela ya dawa kwa kutumia dozi kikamilifu.
Anasema jamii inapaswa kuhakikisha wanapata vipimo na ushauri wa wataalam wa Afya kabla ya kutumia dawa kiholela ambazo zinaweza kuwaletea usugu wa Dawa.
Fimbo anasema Mamlaka yao inandelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaojitokeza kutembelea kwenye Banda la Mamlaka hiyo kwaajili ya kupata elimu kuhusu shughuli wanazozifanya.
“Bado lipo tatizo kwenye jamii ya watanzania kwa baadhi yao kuendelea kutumia dawa pale wanapojisikia kuumwa bila kupima wala kupata ushauri wa Daktari ambapo imewasababishia kupata madhara zaidi kiafya,”anasema na kuongeza
“Bado lipo tatizo katika jamii, watu kutumia dawa kiholela hili ni tatizo ambalo Mamlaka tunaendelea kuwaelimisha wananchi kuwa utumiaji wa dawa kiholela unaweza kusababisha usugu wa bakteria na kufanya dawa hizo kushindwa kufanyakazi ipasavyo” anasema.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa