January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Usalama mahala pakazi ni lazima

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,Ajira na Wenye ulemavu) Mheshimiwa Patrobas Katambi amewataka watu wote wanaomiliki maeneo ya Kazi kuhakikisha yanakuwa salama.

Katambi ametoa kauli hiyo Julai 6, 2023 akizungumza baada ya kutembelea banda la Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pakazi (OSHA) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

“Nitoe rai kwa wamiliki wote wa maeneo ya Kazi, kuhakikisha yanakuwa salama kwa ajili ya kulinda afya ya Wafanyakazi,” amesema Naibu Waziri Katambi na kuongeza,

“Hatuwezi kufanikiwa kama Nchi, kama Wafanyakazi watafanya kazi katika Mazingira yasiyo salama kwani yatahatarisha afya zao,”.

Amebainishwa kwamba changamoto kwa Wafanyakazi ni nyingi ikiwemo kufanya kwazi kwa muda mrefu bila kupimzika na kwenye Mazingira mabaya ambayo kama vile yenye vumbi, vyuma na nyaya za Umeme, vitu ambavyo vinaweza kusababisha ulemavu kwa Wafanyakazi.

Hivyo amewataka wamiliki wa maeneo ya Kazi kushirikiana na OSHA kuhakikisha maeneo yao ya Kazi yanakuwa salama ili kulinda afya ya Wafanyakazi waweze kufanya kazi kwa tija.

Ametumia fursa hiyo kuipongeza OSHA kwa kutumia Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Da es Salaam katika kutoa elimu ya usalama mahala Pakazi kwani watakutana na Watu wengi.