Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline Mbeya
MABADILIKO yaliyofanywa na wanahisa yaliyofanywa na wanahisa hususan Serikali chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mahusiano mazuri na rafiki kwa wawekezaji kupitia falsafa yake ya 4Rs yamewezesha Kampuni ya Saruji Mbeya ambayo pia ni kampuni tanzu ya Amsons kutoa gawio la sh. bilioni 3 kwa Serikali.
Akizungumza wakati wa kikao kifupi na wanahisa na menejimenti kilichofanyika jana kiwandani hapo mwishoni mwa wiki, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, alisema wanajivunia mafanikio hayo.
“Tunajivunia mafanikio haya kwa sababu kwa kipindi cha miaka 10 kampuni hii haikuwahi kutoa gawio kwa wanahisa wake, ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2014 haya ni mabadiliko ya kuungwa mkono,”amesema Mchechu.
Amesema jambo la pili la kujivunia ni kampuni hiyo kuwa kampuni ya kwanza kumilikiwa na kuendeshwa na wazawa, ikiwa ni uwezeshaji uliofanywa na Serikali.
“Serikali kama mmoja wa wanahisa katika kampuni hiyo ikwa na umiliki wa asilimia 25 na kupitia kwa Msajili wa Hazina imepokea kiasi cha sh. bilioni 3 na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wenye hisa asilimia 10 imepokea sh. bilioni 1.2 kama gawio,” amesema.
Pia,ikumbukwe kwamba umiliki wa hisa nyingi za asilimia 65 ndani ya kampuni ya Saruji Mbeya, zilichukuliwa na makampuni ya Amsons ya Tanzania kutoka kwa Holcim ya Uswisi.
Wakizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho mkoani Mbey mwishoni mwa wiki, wanahisa walisisitiza kuendelea kuunga mkono na kuhakikisha kuna ukuaji endelevu kwa miaka ijayo kwa faida ya wadau wote na kuongeza thamani kwa wanahisa wake.
Akizungumza na wafanyakazi kiwandani hapo, Mchechu alisema uwepo wa kiwanda hicho ni maono ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1978, hivyo wanapaswa kuyalinda maono hayo kwa manufaa ya vizazi vyetu.
“Lakini ili tufanye vizuri zaidi tunahitaji kupunguza gharama za uzalishaji ili kukuza faida yetu,” amesema Mchechu
Mbeya Cement Company Limited (MCCL) ilianzishwa nchini Tanzania chini ya Sheria ya Makampuni, 2002 kama kampuni binafsi ambayo inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa saruji.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba