Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
UMOJA wa wanawake wafanyabishara wa sokoni Ilala UWAWASOI wamemchangia shilingi milioni 1 fomu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kugombea urais mwaka 2025 .
WANAWAKE wa Umoja wa Soko la Ilala UWAWASOI walitoa pesa hizo shilingi milioni 1 wakati wa uzinduzi wa umoja huo ambapo walimkabidhi pesa hizo katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala .
Akizungumza katika uzinduzi huo katibu wa UWAWASOI Jane Nyanda, alisema wanawake wa Ilala wanaunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutokana na uchapakazi wake mtetezi wa wanyonge hivyo wanawake wote wa Ilala wanaunga mkono juhudi zake aweze kuendelea miaka mitano tena ya Urais.
“Dkt.Samia Suluhu Hassan ni mwanamke mwenetu na sisi wanawake wa Ilala tumeungana kuunga mkono juhudi zake amefanya mambo makubwa katika jimbo la Ilala katika kumsaidia Mbunge wetu Mussa Zungu ikiwemo sekta ya Afya,sekta ya Elimu ameweza kujenga shule nyingi na vituo vya afya ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na masoko “alisema Jane .
Akizungumzia uzinduzi wa UWAWASOI Katibu Jane Nyanda ,alisema ameanzisha umoja huo kwa lengo la kuunganisha nguvu za Wanawake wafanyabishara katika soko la Ilala na maeneo ya jirani ili kujenga umoja ,mshikamano na katika kushirikiana kukuza soko la Biashara.
Aidha Jane alisema wameweza kupata mafanikio makubwa zaidi wakishirikiana na kusaidiana wao kwa wao pamoja na Serikali na wadau wa Maendeleo.
“Tunashukuru Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono na Jitihada za wanawake katika sekta ya Biashara na kujenga mazingira bora ya kufanya biashara tunaomba Mamlaka husika zitoe ushirikiano zaidi katika kutoa huduma bora za miundombinu, ulinzi na usalama na kutoa fursa sawa za kibiashara kwa wanawake “alisema .
Akizungumzia changamoto alisema ukosefu wa huduma za kifedha ,ukosefu wa mitaji na changamoto ya upatikanaji wa huduma za bidhaa zenye tija,hii inawafanya kuwa tegemezi kwa vyanzo vya fedha visivyo rasmi ikiwemo kukopa Kausha Damu,na hivyo kuathiri ukuaji wa biadhara za wanawake
Changamoto nyingine ukosefu wa elimu na mafunzo ya stadi za biashara na ujasiriamali hii inawafanya kukosa ujuzi muhimu wa kusimamia biashara zao kwa ufanisi na kufanya maamuzi sahihi ya kibiasha na hivyo kutopata tija endelevu za kibiashara .
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto