Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba
Umoja wa bodaboda Bukoba (UBOBU)uliopo Mkoani Kagera unamuomba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,awasaidie kurasimisha biashara ya bodaboda na kutambuliwa kama kundi maalum lenye uhitaji wa kuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara kama walivyofanyiwa Machinga.
Maombi hayo yametolewa umoja huo katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Gymukana Bukoba Mjini uliokuwa ukimpongeza rais na amiri jeshi mkuu wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza bei ya mafuta na kumuomba arasimishe kazi yao ya kuendesha pikipiki.
Katibu wa umoja Salvatory Mlangira ,alisema uendeshaji wa boda boda ni eneo linalotoa ajira kwa kundi kubwa la Vijana Tanzania kwa Bukoba Manispaa kuna madereva bodaboda (8,600).
Mlangira,alisema kundi hilo linawatu wa kada mbalimbali kuanzia elimu ya
msingi hadi elimu ya vyuo vikuu waliokosa ,ajira wote wamejingiza katika sekta hiyo kujiajiri ili waweze kupata kipato kwaajili ya
kuhudumia familia zao za wategemezi wao.
Alisema wakati sasa umefika wa kuitambua rasmi kazi ya uendeshaji wa bodaboda ili kuwa kazi inayotambuliwa kisheria kwa kulinda maslahi yao.
“Kwa sasa tunafanya kazi kwa tabu mmno kutokana na mazingira magumu na mtazamo hasi juu yetu “alisema Mlangira.
Alisema katika kazi hiyo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mikataba umiza wanayopewa na wamiliki wa pikipiki malipo wanayolipa ni mara mbili ya thamani ya pikipiki aliyopewa.
Alisema licha mkataba huo kuwaumiza madereva lakini matengenezo yote pia ni juu yao hali inayopelekea kuendelea kuwa na maisha magumu kwa kukosa pesa za kujikimu na familia zao.
Hata hivyo wamempongeza rasi kwa kuwatua mzigo mzito uliokuwa unalikumba taifa kwa kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na athari za kiuchumi wa dunia zilizochochewa na vita ya Urusi na Ukrain.
Mlangira,alisema hatua ya kupungua kwa bei ya mafuta kulitokana na mtazamo chanya wa serikali ya Samia Hassan kubana matumizi na kutoa ruzuku ya shilingi Bilioni (100)jambo ambalo limesababisha bidhaa hiyo nyeti iliyopanda duniani kote ,kushuka bei hapa nchini kwetu na kusaidia kupunguza ukali wa maisha.
Alisema kabla ya ruzuku lita moja ya mafuta ya petrol Bukoba ilikuwa inauzwa shilingi (3,460)na leo yanapatikana kwa shilingi (3,200)hilo ni mpunguzo la shilingi (260)kwa lita.
Naye mbunge wa jimbo la Bukoba mjini ambaye pia ni naibu waziri wa nishati Wakili Stivene Byabato,alisema rais anajitahidi kwa utu na upendo kushusha bei ya mafuta na wakati huo amehakikisha miradi mingine ya maendeleo inaendelea.
Alisema changamoto nyingine ni wamiliki wa pikipiki kuwa hujumu madereva bodaboda kwa njia mbalimbali ikiwemo kunyang’anywa pikipiki wakati anakaribia kumaliza mkataba kwa kuwekewa vikwazo na hatimaye kukosa haki yake.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba