January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ummy aonya walimu maeneo ya pembezoni kuhamishwa bila kuweka mbadala wake

Ummy aonya walimu maeneo ya pembezoni kuhamishwa bila kuweka mbadala wake

Na Joyce Kasiki,TimesMajira Online,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC) kutohamisha walimu wa maeneo ya pembzoni bila kuweka mbadala ya mwalimu anayehama.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizungumza na Tume ya Utumishi wa walimu jijini hapa.

“Kama mnatoa walimu watano Uvinza nataka.mniambie mmepeleka walimu watano Uvinza,tatizo ninaloliona kila mmoja anataka kufanya kazi Dodoma na maeneo mengine katika halmashauri za mijini.

“Naagiza muwafuatilie na kutoa taarifa ya walimu walioripoti marufuku kubadilisha walimu waliopelekwa maeneo ya pambezoni ..,maana wapo wanaoripoti ili wapatiwe check namba kiisha wanaomba uhamisho,kwa hiyo hili nalipiga marufuku,au ukimtoa mwalimu Ukerewe niambie ni mwalimu gani anaenda Ukerewe” amesema.

Amesema watoto wa wilaya za pembezoni hawatemdewi haki kutokana na walimu wengi kutaka kufanya kazi mijini na kwamba hata wakipangwa katika maeneo ya pembezoni,wanaomba uhamisho.

“Lazima kuwe na uwiano wa walimu wanaohama na kuhamia,najua wana haki ya kuhamishwa lakini nataka nipate taarifa anaenda nani kabla ya kumtoa anayetaka kuhama,” amesema.

Alizungumzia suala la walimu kujiendeleza tofauti na kada ya ualimu ambapo alisema hali hiyo inasababisha kushindwa kuwapandisha madaraja.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu

Amesema kila mwalimu anayetaka kupanda daraja ajiendeleze kwenye kada ya ualimu na siyo kwenda kusomea kada nyingine mje ya ualimu.

“Walimu wajiendeleze katika kada ya ualimi ili kurahisisha upandishwaji wa madaraja wapo walimu wanaoenda kusomea au kujiendeleza kwa kada nyingine tofauti na ualimu,inakuwa ngumu katika suala la kuwapandiaha madaraja pindi wanapohitimu masomo yao,” amesema.

Katika hatua nyingine ameiasa Tume hiyo kushughulikia malalamiko ya walimu bila upendeleo wowote .

Akizungumzia mafanikio ya Tume hiyo tangu ilipoanza kutekelezwa majukumu yake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Paulina Mkwama amesema malalamiko mengi ya watumishi walimu yameshughulikiwa ikiwemo suala la ajira,kupanda vyeo ,kuthibitishwa kazini ,kubadilisha vyeo na kupatiwa vibali vya kustaafu.

Vilevile amesema masuala ya nidhamu yanashughulikiwa kwa wakati kulingana na mashauri yanavyojitokeza.

Aidha baada ya mazungumzo na TSC Waziri Ummy alikabidhi pikipiki 75 kwa Makaimu Makatibu wasaidizi wa Tume hiyo kwa ngazi ya wilaya ili ziweze kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.