November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ummy akagua maandalizi maadhimisho siku ya mashujaa

Na Mwandishi wetu – Dodoma

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga leo tarehe 10 Julai, 2024 amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa inayotarajiwa kufanyika 25 Julai, 2024 jijini Dodoma.

Akozungumza mara baada ya ukaguzi huo Ummy amesema ni imani yake kwamba maandalizi hayo yatakamilika kwa wakati.

Aidha, maadhimisho hayo yatashirikisha gwaride la Majeshi ya Ulinzi na Usalama lenye vikosi vitano ambavyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Poliosi, Jeshi la Magereza pamoja na jeshi la Uhamiaji.

Awali akitoa maelezo kuhusu maandalizi hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Batholomeo Jungu amebainisha kuwa, maadhimisho hayo yatatanguliwa na uwashaji wa Mwenge 24 Julai, 2024 usiku ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatafanyika 25 Julai, 2024 jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan.