December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ulega aipeleka tuzo ya heshima kwa Rais Samia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake kwa wadogo anaipeleka kwa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa yeye ana utashi wa kisiasa ya kutaka kuona sekta ya uzalishaji inasonga mbele.

Ulega amesema hayo kwenye Mkutano wa Wavuvi Wadogo Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 5-7,2024.

Mapema leo katika mkutano huo, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Afrika linaloshughulikia Tafiti, Haki za Wanyama na sekta ya Uvuvi (AU-IBAR), Bi. Hellen Guebama alimkabidhi tuzo Waziri Ulega ikiwa ni ishara ya kumpa heshima na kutambua mchango wake kwenye shughuli za uvuvi mdogo nchini.