April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

IMEELEZWA kuwa ulaji wa vyakula vya aina moja,kurithi matatizo ya macho na umri vimetajwa kuwa changamoto kubwa ya magonjwa ya macho kwa wananchi jijini Mbeya na maeneo mengine.

Hayo yamesemwa leo April 18,2025 na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt.Yesaya Mwasubila wakati  wa zoezi la upimaji macho ambalo linafanyika kwa siku tatu Jijini Mbeya.

Zoezi hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust kupitia Mkurugenzi wake,  Spika wa Bunge na Mbunge  Jimbo la Mbeya  ambaye pia, Rais Umoja wa Mabunge Duniani(IPU Dkt.Tulia kwa kushirikiana na The Muslim  Mission of Tanzania.

Katika kambi hiyo ,Spika wa Bunge ,Dkt ,  Ackson ameongoza  maelfu ya wananchi katika zoezi hilo  katika Shule ya Msingi Kagera, iliyopo Kata ya Ilomba ambalo  limeanza April 18 mpaka  April 21 mwaka huu.

Imeelezwa  huduma hiyo ya macho inatolewa bila malipo kupitia Taasisi ya Tulia Trust kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya.

Dkt.Mwasubila amesema  Halmashauri ya jiji la Mbeya tatizo la macho ni kubwa na kuwa inaweza kuwa si halmashauri ya Jiji pekee bali katika mikoa mingine.

“Kuna baadhi ya vyakula vimekosa viiini lishe kwa ajili ya kuwezesha uonaji wa macho vizuri kuna vitu vinaitwa karoti kuna vitamini A  ambazo zinachangia mtu kuona vizuri ,sasa wengine wanakosa kula vyakula vyenye vitamini A Sasa hii inaweza kuathiri hasa  waliopo mashuleni,”amesema

Kuhusu magonjwa yasiyoambukiza yanaenda kadri umri unavyo ongezeka na aina ya vyakula vinavyoliwa yote hayo yanaathiri kutokuona vizuri

Amefafanua  ni lazima wananchi waelimishwe namna ya vyakula ambavyo vinafaa hasa kwa vijana wa shule na kwamba kutokana na uchumi wa  kila shule hivyo   baadhi ya shule kula vyakula vya aina moja .

Kwa upande wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia  Ackson amewasihi wananchi wa  kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo muhimu kwa afya zao.

Amesema dhamira ya Taasisi ya Tulia Trust katika kuboresha ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Aidha amesema jumla ya watalaam 67, wamekuja kutoa huduma ya matibabu ya macho ,miwani na upasuaji na kusema Tulia Trust kazi yao ni kuhakikisha wapo kutoa huduma.

“Kwa hiyo ndugu zangu hawa ni watu ambao wanajitoa sana na kuaminika  pamoja na sisi kujitokeza  wanapata heshima mbele za Mungu , lakini mbele za wanadamu pia hivyo wakienda huko wanasema nini mnaona idadi kubwa ya watu “amesema Dkt Tulia

Kwa upande wake Mratibu wa  kambi ya macho macho  wa Bilal  Muslim,  Ain Sharif amesema   Dkt  Tulia anafanya jambo la kimungu na kumhakikishia kuwa zoezi  hilo watalifanya kwa uhakika na kwa wakati.