December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ukarabati MV Magogoni kukamilika Disemba 2024

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

SERIKALI imesema ukarabati wa Kivuko cha Mv. Magogoni unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Desemba, 2024 na kurejeshwa Nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Bungeni  na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile aliyeuliza ni lini matengenezo ya Pantoni ya Mv. Magogoni iliyopo nje ya Nchi yatakamilika na kurejeshwa nchini ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Itaumbukwa kuwa Mwezi Februari 2023 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ilisaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.5.

Lengo la ukarabati huo wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini, kuharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine.