Na mwandishi wetu, TimesMajira Online Loliondo, Ngorongoro
Kamishina wa Uhamiaji anaehusika na Udhibiti wa mipaka Tanzania CI Samwel Mahirane amesema wao kama idara ya Uhamiaji wamepokea maelekezo ya waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Eng.Hamad Yusuf Masauni katika zoezi linaloendelea la uwekaji mipaka katika Pori tengefu la loliondo.
Kamishina Mahirane amesema tayari wameshawatambua watu ambao wamehusika na hujumu katika zoezi la uwekaji wa mikapa katika pori tengefu la Loliondo
Kamishina Mahirane amesema idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalam tayari wameanza uchunguzi wa watu waliotajwa kuhujumu zoezi kama ni raia wa Tanzania ama si watanzania hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“muda wowote kuanzia sasa tutawakamata na kama ni watanzania wamekwenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu hatua sitaiki zitachukuliwa dhidi yao” alisema kamishina wa uhamiaji anaeshughulika na udhibiti wa mipaka Tanzania.
Pia amesema “kama kuna Mtanzania aliyeujumu zoezi hili na akakimbilia nchi jirani ni vyema akajitokeza vinginevyo tutawakamata kwa sababu taarifa tu nazo” alisema kamishina udhibiti wa mipaka idara ya uhamiaji Tanzania
Aidha amesema asasi za kiraia ambazo zinafanya kazi katika wilaya ya Ngorongoro na Tanzania ambazo zilijisajili kwa lengo la kusaidia jamii zinakwenda kuchunguzwa upya ili kubaini uhalisia wa kazi wanazofanya kama alivyoelekeza waziri wa mambo ya Ndani ya Nchini.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato