Na David John, TimesMajira Online
BAADA ya Rais Samia Suluhu Hassani kufanya ziara nchini Ufaransa ambayo imekuwa na mafanufaa makubwa,Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui amesema ziara hiyo imefungua fursa mbalimbali ambazo zitaendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari Balozi Nabil amesema katika ziara hiyo Rais Samia na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamepata fursa ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo, uchumi na dplomasia.
Amesema katika mazungumzo yao marais hao pia wamejadiliana kuboresha ulinzi na utunzaji wa bahari ikiwa ni mkakati wa kufikia uchumi wa bluu,miundombinu ya usafirishaji ikiwemo katika majiji makubwa hasa Dar es Salaam.na wamezungumzia kuimarisha sekta ya kilimo na uchukuzi.
Pia amesema marais hao wamejadiliana kuhusu uwekezaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili sambamba na kuendelea kukuza diplomasia.”Tunampongeza Rais Samia kwa kufanya ziara katika nchi yetu ya Ufaransa kwani imekuwa na mafanikio makubwa, imefungua fursa mbalimbali nakwamba Rais Samia mabadiliko makubwa.”
Akifafanua zaidi kuhusu ziara hiyo amesema Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD wameingia makubaliano ya kutia saini mikataba mitatu ya miradi ya maendeleo yenye ufadhili wa jumla ya Euro milioni 259.Miradi hiyo itajikita katika sekta ya kilimo, uchukuzi na miundombinu pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Nabil ameongeza kwamba nchi ya Ufaransa na Tanzania zitaendelea kushirikiana na hivi karibuni Tanzania inatarajia kupokea jopo kubwa la ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini humo ambapo kwa pamoja watakutana na mamlaka zinazohusika na masala ya kibiashara kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji utakaokuza uchumi na maendeleo.
“Wafanyabiashara hao wakiwa hapa nchini pamoja na kukutana na viongozi wa kiserikali watakuwa na ratiba ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.Wafanyabiara hao kutoka nchini Ufaransa wakiwa hapa Tanzania watakuwa na programu maalumu ya kuwainua wajasiriamali wachanga”amesema Balozi Nabil.
Rais Samia alikwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya kushiriki kilelele cha mkutano wa wakuu wa nchi zilizopo ukanda wa bahari kufuatia mualiko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.Pia Rais Samia alipata nafasi ya kuhutubia mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza umuhimu wa yeye kupata elimu inayohusu utawala wa bahari na rasilimali zake.
Pia Rais katika hotuba yake alisema kwamba Tanzania itanufaika kwa kupata teknolojia na miundo bora ya kiuendeshaji wa bahari ili kufikia uchumi wa bluu.
Katika hatua nyingine balozi huyo amekutana na kufanya mzungumza na maofisa na watumishi wa ubalozi huo ambao wamekwa msaada mkubwa katika kufanikisha ujumbe wa serikali yaTanzania uliombatana na Rais wa Tanzania kufanikisha ziara yake nchini ufaransa.
mwisho wa Ufaransa Emmanuel Macron wamepata fursa ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo, uchumi na dplomasia.
Amesema katika mazungumzo yao marais hao pia wamejadiliana kuboresha ulinzi na utunzaji wa bahari ikiwa ni mkakati wa kufikia uchumi wa bluu,miundombinu ya usafirishaji ikiwemo katika majiji makubwa hasa Dar es Salaam.na wamezungumzia kuimarisha sekta ya kilimo na uchukuzi.
Pia amesema marais hao wamejadiliana kuhusu uwekezaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili sambamba na kuendelea kukuza diplomasia.”Tunampongeza Rais Samia kwa kufanya ziara katika nchi yetu ya Ufaransa kwani imekuwa na mafanikio makubwa, imefungua fursa mbalimbali nakwamba Rais Samia mabadiliko makubwa.”
Akifafanua zaidi kuhusu ziara hiyo amesema anashukuru kuona Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD wameingia makubaliano ya kutia saini mikataba mitatu ya miradi ya maendeleo yenye ufadhili wa jumla ya Euro milioni 259.Miradi hiyo itajikita katika sekta ya kilimo, uchukuzi na miundombinu pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Nabil amesema kwamba nchi ya Ufaransa na Tanzania zitaendelea kushirikiana na hivi karibuni Tanzania inatarajia kupokea jopo kubwa la ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini humo ambapo kwa pamoja watakutana na mamlaka zinazohusika na masala ya kibiashara kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji utakaokuza uchumi na maendeleo.
“Wafanyabiashara hao wakiwa hapa nchini pamoja na kukutana na viongozi wa kiserikali watakuwa na ratiba ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.Wafanyabiara hao kutoka nchini Ufaransa wakiwa hapa Tanzania watakuwa na programu maalumu ya kuwainua wajasiriamali wachanga”amesema Balozi Nabil.
Rais Samia alikwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya kushiriki kilelele cha mkutano wa wakuu wa nchi zilizopo ukanda wa bahari kufuatia mualiko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.Pia Rais Samia alipata nafasi ya kuhutubia mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza umuhimu wa yeye kupata elimu inayohusu utawala wa bahari na rasilimali zake.
Pia Rais katika hotuba yake alisema kwamba Tanzania itanufaika kwa kupata teknolojia na miundo bora ya kiuendeshaji wa bahari ili kufikia uchumi wa bluu.
Wakati huohuo balozi huyo amekutana na kufanya mzungumza na maofisa na watumishi wa ubalozi huo ambao wamekwa msaada mkubwa katika kufanikisha ujumbe wa serikali yaTanzania uliombatana na Rais wa Tanzania kufanikisha ziara yake nchini ufaransa.
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba