December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uchumi wa Bandari inatekeleza miradi ya Maendeleo Nchini

Na Heri Shaaban. (Ilala)

Uchumi wa Bandari ya Dar es Salaam unatekekeza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika miradi ya Maendeleo Nchini .

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Bandari nchini TPA Mlisho Selemani Mrisho ,wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Mchafukoge walivyofanya ziara Bandarini hapo kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mariam Lulida.

“KUKUA Kwa uchumi wa Bandari ya Dar es Salaam kunatekeleza Ilani ya chama katika kujenga miradi ya Maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya ,Elimu ,Miundombinu inategemea uchumi wa Bandari yetu ” alisema Mrisho .

Mkurugenzi wa Bandari Mrisho alisema wana Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania TPA ambapo alisema TPA I
ina Bandari za Bahari Dar es Salaam inafuata na Tanga, Mtwara na Bandari ndogo Bagamoyo na zingine .

Aidha alisema Bandari zingine za maziwa Ziwa Tanganyika ,ziwa Victoria na ziwa Nyasa na Bandari kubwa Dar es Salaam ndio chanzo cha uchumi wa mapato ya Tanzania ambapo Bandari hiyo ina kusanya kodi na tozo mbali mbali .

Mrisho alisema mwaka 2022 meli za shehena ziliongezeka pamoja na Mapato malengo ya TPA kwa mwaka 2023 Tani milioni kumi Mpaka kuvuka malengo kufikia Tano milioni 20 .

” Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaitazama Bandari kwa ukaribu ndio Chachu ya mapato ya nchi shule ,vituo vya afya hosipitali zote zinajengwa kwa ajili ya kutegemea vyanzo vya mapato ya Bandari ya Dar es Salaam “alisema .

Diwani wa Kata ya Mchafukoge Maliam Lulida alisema katika Ziara hiyo na Kamati ya Siasa ya Mchafukoge yupo na kamati yake ya Siasa ya CCM wamefarijika ziara hiyo Katika madhimisho ya ccm kutimiza miaka 46 wanaangalia utekelezaji wa Ilani wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan .

Diwani Lulida alisema dhumuni la Ziara hiyo katika Bandari hiyo kuangalia Utendaji wa KAZI na kujifunza na kujionea Ili waweze kwenda kuwaeleza Wananchi Bandari inavyofanya kazi.

“Chama Cha Mapinduzi CCM Mchafukoge tumejilidhisha na Kamati yangu ya Siasa bandari yetu ya kisasa mitambo ya kisasa imewekwa na Rais wetu wa awamu ya sita Ina uwezo wa kushusha gari laki sita kwa siku sehemu ya kujivunia

Katibu wa Siasa na U wenezi wa CCM Kata Mchafukoge Mshokery Mandary amempongeza Serikali kwa upanuzi wa Bandari yetu kwa Sasa Ina uwezo wa kupokea meli nyingi gata mpya zimefungwa na Ina uwezo wa kuhudumia Afrika Mashariki yote amewataka Watanzania kufanya Ziara na kujifunza wasilishwe matango poli na kudanganywa.

Diwani wa kata ya Mchafukoge Wilayani Ilala Mariam Lulida (katikati)akiwa katika ZIARA Bandari ya Dar es Salam Leo January 31/2023 katika madhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa CHAMA Cha mapinduzi CCM na kuangalia utekezaji wa Ilani ya CHAMA Cha mapinduzi (Kushoto )madiwani wa viti Maalum Wilaya ya Ilala Batuly Mziya na Aisha Kipini na viongozi wa Bandari (Picha na Heri Shaban)
DIWANI wa kata ya Mchafukoge Mariam Lulida akizungumza na waandishi wa habari makao Makuu ya Bandari Dar es salaam
DIWANI wa kata ya Mchafukoge Mariam Lulida akiwa kamati ya siasa ya Mchafukoge katika ziara Bandarini Dar es Salaam katika kuazimisha miaka 46 ya kuzaliwa CCM PICHA NA HERI SHAABAN.