Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma
UCHAGUZI Mkuu wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NaCoNGO ) unatarajiwa kufanyika Julai 8,mwaka huu mkoani Dodoma.
Hatua hiyo imekuja kutokana na hivi karibuni Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima kutoa maagizo kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa baraza hilo na kuunda kamati ya watu 10 kwa ajili ya kusimamaia uchaguzi wa baraza hilo ambalo lilipewa muda wa siku 30.
Hayo yameelezwa jijini hapa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya NaCoNGO,Wakili Flaviana Charles wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya mwenendo wa uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ngazi ya Wilaya (NaCoNGO).
Amesema, Uchaguzi wa Baraza hilo hususan katika Ngazi ya Wilaya, ulifanyika Juni 26 Mwaka huu,na kwa ujumla, zoezi hilo lilifanyika kwa amani na utulivu katika Wilaya zaidi ya 130 za Tanzania Bara.
“Uchaguzi ulisimamiwa na viongozi wa mashirika yaliyoshiriki uchaguzi katika ngazi ya wilaya. Wasajili wasaidizi wa wilaya nao walishiriki kama waangalizi wa uchaguzi katika ngazi hizo. 5.0 Kutangaza Mshindi wa Uchaguzi Kama ilivyofanyika katika zoezi la kupiga na kuhesabu kura, Wagombea watatu (03) walioongoza kwa kura nyingi, walitangazwa kuwa washindi katika ngazi ya Wilaya na kujazishwa Hati ya Kiapo cha Kiongozi wa Baraza, kama ilivyoainishwa na Kanuni ya 17 (1) ya Kanuni za Uchaguzi za Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali za mwaka 2016,”amesema.
Aidha, amesema kati ya watia nia watano waliochukua fomu za kuomba uongozi wa Baraza, jumla ya watia nia wanne walirudisha fomu hizo kwa msingi huo, zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lilifanikiwa kwa takribani asilimia 80.
Pia kupiga na kuhesabu kura zoezi lilifanyika tarehe 26 Juni, 2021 katika wilaya zote ndani ya mikoa 25 ya Tanzania Bara, isipokuwa katika wilaya za Mkoa wa Kigoma, ambako kwa sababu zilizokubalika na pande zote (Wasimamizi wa Uchaguzi, Wagombea na Wapiga Kura).
Amebainisha kuwa, uchaguzi katika ngazi ya mikoa yote unafanyika kuanzia leo tarehe 28/06/2021 hadi tarehe 02/07/2021huku wasajili wasaidizi ngazi wa mikoa watakuwa waangalizi huru wa uchaguzi katika mikoa husika.
Baraza la NacoNGO litakaloundwa litakuwa na wawakilishi/wajumbe 30, kati yao wajumbe 26 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara; (Mjumbe mmoja kutoka kila mkoa) na wajumbe wanne watachaguliwa kutoka katika makundi maalumu na makundi hayo ni pamoja na mashirika ya kimataifa, watu wenye ulemavu, watoto na vijana.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi