Na David John,Timesmajira,online
SERIKALI ya Ufaransa kupitia ubalozi wake nchini Tanzania umetoa sh. bilioni 1.7 kwa lengo la kusaidia makundi ya Wanawake, wasichana na vijana ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha hususani kwenye sekta ya kilimo.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar Es Salaam Balozi Fr’de’ric Clavier amesema kuwa Ufaransa wametoa fedha hizo kupitia mashirika matatu yanayofanya kilimo endelevu nchini.
Amesema Serikali ya Ufaransa imetoa fedha hizo Kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Empowerment through Agroecology na permaculture Gape ambapo ufaransa itaendelea kusaidia eneo la usawa wa kijinsia na mabadiliko ya tabia ya nchi na kukabiliana nayo.
” Katika kusaidia hili Serikali ya Ufaransa Kwa hapa Tanzania tumeleta mradi huu wa miaka miwili ambapo unajulikana kama Gape wenye thamani ya sh.Bilioni 1.7 na lengo kubwa ni kuwahamsisha na kuwawezesha wasichana 2000 ambao ni sawa na asilimia 90 na wavulana asilimia 10 katika kilimo cha mboga mboga.”amesema Balozi Clavier
Amesema kuwa vijana hao wakike kwa waume watatoka katika mikoa ya Tabora, wilayani Nzega ,Mkoa wa Dodoma wilayani Kongwa na Zanzibar na kwamba mradi huo ni mwendelezo wa mradi wa kwanza uliopewa jina la Agroecology .
“Utunzaji huu na usaidizi kwa wakulima wadogo kwa ajili ya kilimo hai .Serikali ya Ufaransa itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania katika mapinduzi ya kilimo cha kisasa ili kuwa na kilimo endelevu kitakachofikia malengo.” Amesisitiza Clavier
Amefafanua kuwa asilimia 80 ya wakulima wadogo ni wanawake ambao wanapitia wakati mgumu na mazingira magumu ya kupata Ardhi Kwa ajili ya kilimo .
Ameongeza kuwa katika kupambana na hilo ubalozi wa Ufaransa unasaidia mashirika manne ambayo ni FCST rust, Msichana Initiative,PPIZ na SAT ambayo yote yanafanya kazi Kwa pamoja kuwafundisha wasichana kilimo endelevu na haki zao kwa lengo la kuongeza uzalishaji uwingi na ubora.
Wakiishukuru Serikali ya Ufaransa kupitia ubalozi wake hapa nchini wakurugenzi wa mashirika hayo hapa nchini walisema kuwa wanaamini kupitia mradi huo wa Gape wasichana na vijana watakwenda kufikiwa na kunufaika moja Kwa moja.
“Mradi huu utakwenda kuwanufaisha vijana na wasichana hususani waliotajwa katika mikoa ya Dodoma ,Tabora na Zanzibar zaidi ya 1000 na Kwa Zanzibar ni vijana 820 watanufaika na mradi huu moja Kwa moja.” amesema Rebbeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika Msichana Initiative.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam