Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SHIRIKA linalojishughulisha na masuala ya Vijana Tanzania Youth Coalition (TYS),imejipanga kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu kupitia mitandao mbalimbali ili waweze kukuza biashara zao.
Akizungumza kwenye maonesho ya 48 ya Biasharaya Kimataifa yanayoendelea ,Ofisa Utekelezaji wa Mradi wa Boresha Maisha Vijana uliofadhiliwa na Shirika la We Effect na kutekelezwa na TYC,Josephine Onesmo amesema changamoto kubwa ya vijana wanayokutana nayo,ukiachilia mbali suala la mitaji wanakosa kujua ni namna gani wanaweza wakatafuta masoko mbali na eneo ambalo wanaishi.
Amesema mwaka huu wameamua kuwaleta vijana kutoka maeneo mbalimbali katika maonesho ya Sabasaba kwa lengo kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali ambazo wanazifanya kuweza kupata elimu na kutambua fursa zingine katika kukua katika masuala ya utunzaji wa fedha,elimu kuwekeza ,kujiunga na vikundi.
Pia amesema watapata uelewa wa kujua mifumo mbalimbali ya biashara itakayofanya wakuwe katika masuala ya masoko ya kimtandao katika kukuza biashara zao.
“TYC inawanachama mbalimbali ambao ni taasisi za vijana lakini zinafanya kazi na vikundi vya vijana ambao ni wajasiriamali na vijana wakulima, katika utekelezaji wa mradi huu moja ya malengo ni kuwajengea uwezo vikundi vya vijana wajasiliamari lakini wanachama wa tyc kuwa na mifumo bora ya uendeshaji wa taasisi na vikundi vyao na kupata fursa mbalimbali za kibiashara katika vikundi vinavyofanya ujasiriamali na shughuli za kilimo,”amesema na KuongezaÂ
“Sabasaba hii tumekuja na vikundi kutoka Mkoa wa Iringa na Dodoma ambao ni wanachama wa TYC ,Pia tumekuja na Vijana wajasiliamari kutoka Kilimanjaro ambao wamekuja na bidhaa mbalimbali,”amesema.Â
Kwa upande wake Ofisa Utekelezaji Mradi wa USAID Kijana Nahodha (YOUNG CAPTAIN) , uliofadhiliwa na USAID na kutekelezwa na Taasisi ya TMARC-Tanzania na washirika wenza TYC pamoja na Shirika la Kimataifa la Care na Ylabs,Salma Kagya amesema vijana nguzo imara katika kujenga taifa hivyo ni vema kuhakikisha wanawekewa mazingira bora.
Amesema vijana ni asilimia kubwa sana Tanzania ambao wanakiu ya kupata fursa mbalimbali “Mradi huu unawafanya vijana kujitambua zaidi waweze kuwa na afya bora na kuwa na ushiriki bora katika jamii,”amesema.
Amesema mradi huo wa Nahodha ni wa vijana umri kati ya miaka 15 hadi 25 unaoendeshwa katika maeneo matatu Dares Salaam,Morogoro na Zanzibar .
“Mradi huu unajumla ya vijana wanaotarajiwa kufikiwa ni 45000 ambapo ndani ya hiyo vijana hao wapo katika vikundi wanajiendeleza kiuchumi lakini pia sabasaba tupo na vijana hao ambao wamekuja na bidhaa ambao wamezibuni wenyewe,”amesema.
Amesema vijana hao katika mradi huo wamekuja kujitafutia kipato kwa kuuza bidhaa zao zkama Mkaa Mbadala ,Majiko Sanifu ,bidhaa ambazo za kidigital i,mafuta ,sabuni za mwani na mafuta ya nazi,picha wachoraji.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato