January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Twanga Pepeta waikubali ‘Speed’ ya Rais Samia

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Dar

MMILIKI wa bendi ya Twangapepeta nchini, Asha Baraka ameiomba serikali kupitia Basata, kutoa fursa za mialiko katika shughuli na matukio mbalimbali yanayoratibiwa na Serikali ya awamu ya sita.

Lengo la kutoaka mialiko hiyo kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuonesha umahiri wao wa kustawisha muziki wa dansi nchini.

Asha Baraka ameyasema hayo alipotembelea na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Basata, Dkt. Kedmon Mapana ofisini kwake Aprili 08 mwaka huu.

Hata hivyo, Asha Baraka aliambatana na Mkurgenzi wa Bendi hiyo Luiza Mbutu na Meneja Hasan Rehani ambapo alifurahishwa na “speed” ya Serikali kwenye kuinua sekta ya sanaa nchini.

“Tumechangia mambo mengi ya uendeshaji wa sanaa nchini na sisi kama Twanga, tunaleta maombi yetu kwake, aangalie muziki wa dansi uweze kukua na hizi kazi za serikali tuweze kusimamiwa tuzipate kwakuwa imedhamiria kuinua sanaa,” alisema Asha Baraka.

Ameongeza kuwa, Baraza lifanye utaratibu kama wanavyofanya kwa sanaa zingine kwa kuwaombea kibali cha kutembelea Ikulu ili kumsalimia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.