July 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TUREFO waeleza mikakati ya kusaidia jamii

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

TAASISI ya TUMANYILE Relief Foundation (TUREFO) yaeleza mikakati yake kwa ajili ya kusaidia jamii kwa kukuza upendo kwa ajili ya ustawi na wema kwa wahitaji kupitia ushirikiano na Taasisi husika na za kiserikali .

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Rachel tawi Malimbwi, wakati wa madhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kata ya CHANIKA Wilayani Ilala.

“TUREFO mikakati yetu kukuza upendo kwa ustawi kutoa misaada,ushauri nasaha chakula,dawa ,nguo na malazi kwa majanga mbali mbali kwa ajili ya kuisaidia Serikali ” alisema Rachel.

Mkurugenzi Rachel alisema mikakati mingine kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi,Uwezeshaji,ufahamu ,na kuimalisha uwezo Muungano wa mikakati na kugawa Rasilimali.

Aidha pia alisema TUREFO ina lenga kupunguza umasikini fursa sawa na maisha endelevu kwa watoto,vijana,wanawake Wazee ,walemavu na kutafuta rasilimali muhimu .

“Lengo la shirika letu Tumanyile Relief Foundation TUREFO ni shirika jipya lisilo la Kiserikali lililoundwa na Wanachama waanzilishi kumi Mwezi October 2022 ni shirika lisilo la kiserikali wala sio la kidini ” alisema