Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KATIKA kuendelea kukuza biashara za kimtandao ,Kampuni inayotumia teknolojia kutatua matatizo ya watu yanayohusiana na Malipo Tunzaa Fintech pamoja na Kampuni ya simu Vodacom kupitia M-pesa zimekuja na njia salama, ambayo itawawezesha wateja kupata huduma mbalimbali kwa kulipa kidogo kidogo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza ushirikiano huo Mkuu wa Kitengo cha Wateja TUNZAA, Abdallah Said amesema wameamua kuja na suluhisho rahisi kwa watanzania kwa ajili ya kuwawezesha kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ambazo watazihitaji kwa kudunduliza .
Amesema kupitia Tunzaa mtumijaji wa M Pesa ataweza kununua bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa ya nyumbani pamoja na vifaa vinginevyo.
” Kwa sasa wateja wa Mtandao wa Vodacom kupitia huduma ya Mpesa wataweza kufanya miamala yao na kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogo kidogo kutoka kwenye Aplikesheni ya Tunzaa itakayokuwa ndani Aplikesheni ya M-pesa,”amesema.
Alibainisha kuwa lengo la Tunzaa ni kuimarisha tabia chanya za kifedha kwa waafrika wa kila siku kwa kuwawezesha kununua bidhaa kwa awamu bila madeni.
“Hivi sasa watumiaji wa Tunzaa wanaweza kununua bidhaa mbalimbali kwa kududuliza ikiwemo vifaa mbalimbali vya nyumbani na vifaa vingine,”amesema.
Mkuu huyo wa kitengo cha wateja amesema kwa sasa Tunzaa imekuwa ikitoa huduma zake Tanzania nzima huku ikijipanga kutatua wigo kufikia nchi jirani kama Kenya, Uganda, Zambia ,Kongo, msumbiji na badae kufikia nchi zote za kiafrika.
Akitaja faida muhimu ambazo watumiaji watapata kupitia Tunzaa, Said ……….amesema aplikesheni hiyo ina usalama,uwezo wa kupata bidhaa kwa urahisi zaidi pamoja na uhuru wa kifedha ulioboreshwa.
Kwa upande wake Meneja Malipo ya Kidigitali na chaneli za mtandaoni kutoka Vodacom M- pesa, Josephine Mushi amesema ushirikiano baina yao na Tunzaa ni dhihilisho kua Vodacom imeendeleza kauli mbiyu yake ya pamoja tunaweza .
Amesema ushirikiano huo utawawezesha wateja wake kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogokidogo mara baada ya kuhifadhi fedha zake Tunzaa.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua