Na Steven Augustino,TimesMajira Online. Tunduru
SERIKALI ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, imesema bei elekezi ya saruji wilayani hapa ni sh. 14,500 kwa mfuko mmoja na mfanyabiashara yeyote atakayekiuka maelekezo hayo na kuuza juu ya bei hiyo, atakamatwa na kushtakiwa.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa wadau wa usafirishaji uliofanyika kwenye viwanja vya Balaza la Idi mjini hapa ambapo hali hiyo, imetokana na serikali kubaini uwepo wa wimbi kubwa la wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kupandisha kiholela.
Mtatiro amesema katika wilaya yake, wapo wafaanyabiashara ambao wamekuwa wakiuza bidhaa hiyo kati ya sh. 15,000 hadi sh. 18,000 kwa mfuko mmoja na tayari ameanza kuwakamata na wote watafunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Amesema kwa sasa wapo wafanyabiashara, ambao walikuwa wanatumia vibaya na kujinufaisha kutokana na kufungwa kwa ajili ya ukarabati wa kiwanda cha Dangote na kwamba taarifa alizonazo hivi sasa, kiwanda hicho kimeanza uzalishaji hivyo siku chache zijazo upungufu wa saruji uliopo utakwisha.
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunziÂ
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu