
Na Mwandishi Wetu.
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacob Mwambelege, amesema Tume za uchaguzi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimekutana kujadili mafanikio na changamoto za uendeshaji wa uchaguzi, kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mifumo ya uchaguzi na demokrasia katika ukanda huo.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 28 wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC), uliofuguliwa Novemba 23 na Waziri Mkuu Dkt Mwingulu Nchemba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jaji Mwambelege amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa nchi wanachama kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kusimamia na kuendesha uchaguzi.

“Jukwaa hili limekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uwezo wa tume za uchaguzi kupitia mafunzo, warsha, mikutano na ziara za kujifunza kutoka kwa tume nyingine wanachama”amesema
Aidha, amesema kupitia ushiriki katika shughuli mbalimbali za jukwaa hilo, INEC Tanzania imepata fursa ya kushiriki katika misheni za uangalizi wa uchaguzi ndani na nje ya ukanda wa SADC, pamoja na kutembelea tume nyingine kwa ajili ya kujifunza masuala ya kiutendaji.⁸

Aidha amesema mkutano huo umekutanisha washiriki zaidi ya 108 kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika, wakiwemo wenyeviti na makamishna wa tume za uchaguzi, watendaji wakuu na maafisa waandamizi kutoka tume 15 za uchaguzi za nchi wanachama 14 wa SADC pamoja na Sekretarieti ya ECF-SADC.


More Stories
Kafulila:Sekta binafsi ishiriki kilimo cha umwagiliaji
Kafulila:Tanzania kujiandaa na ongezeko la watu 2044
Daraja Lubanda ni imara, salama kwa watumiaji: Tanroads