June 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tume ya nguvu za Atomic wakutana na wadau wa nishati kujadili umeme wa nyukilia

Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)

TUME ya Nguvu za Atomiki
wakutana na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati kwa ajili ya kujadili na kupata matumizi salama ya nguvu za umeme wa nyukilia. .

Akizungumza katika mkutano huo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya nguvu za Atomic Tanzania Profesa,Joseph Msambichaka,alisema umeme wa nyukilia uanza kwa gharama kubwa wakati wa kuweka kwa ajili ya matumizi baadae una faida

“Umeme wa nguvu za nyukilia unazalishwa nchini na Tume ya nguvu za Atomic wadau mbalimbali wamekutana kujadili masuala ya nguvu za Atomic” alisema Msambichaka

Profesa Msambichaka, alisema umeme wa nguvu za nyukilia una faida kubwa na unatumika bila madhara .

Kwa upande wake Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa umeme nishati jadilifu,kutoka Wizara ya Nishati alisema wanakutana kwa ajili ya kuendeleza rasilimali za umeme wa nguvu za nyukilia .

Mhandisi Innocent Luoga alisema kwa kushirikiana na Tume za nguvu za Atomic Tanzania imeleta wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuzalisha umeme wa nyukilia mradi wa rasilimali ya nchi yetu.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwezesha rasilimali ya mradi wa nguvu za nyukilia kwa maelekezo ya Rais Dkt.Samia,ambapo wataalam wapo mbalimbali nyukilia wameshiriki mkutano huo.

Alisema nchi yetu inajifunza kutoka kwa nchi jirani kutumia umeme wa nguvu za atomic mkutano huo pia umeshirikisha wataalam wa OSHA,Baraza la Hifadhi Mazingira na wadau wengine.

Murugenzi Mkuu wa Tume za Nguvu za Atomic Tanzania,Profesa Najat Kassim Mohamed,alisema mkutano huu ni muhimu sana katika nchi yetu wanakutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kupata matumizi salama ya nguvu ya nyukilia.