September 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia aibana hospitali, maiti kukaa zaidi ya mwezi

Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Mbeya

KATIKA hali isiyo ya kawaida wananchi wa kata ya Igawilo halmashauri ya Jiji la Mbeya wamemtumia ujumbe wa njia ya simu Mbunge wa Mbeya mjini na spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson kulalamikia mradi wa jengo la watoto kutumika kama stoo sambamba na maiti ya mwanaume mmoja asiyejulikana mwili wake kuhifadhiwa chumba cha maiti kwa muda wa mwezi mmoja.

Spika wa Bunge Dkt.Tulia amefika katika hospitali ya Igawilo kupanda miti katika eneo la hospitali akiwa ameongozana na baadi ya wananchi ndipo baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti alipopata kero za wananchi zilizotumwa kwa njia ya simu yake ya mkononi wakielezea kero zilizopo katika hospitali hiyo.

Akiendelea kusoma kero hizo za wananchi Dkt. Tulia alisema kuwa changamoto nyingine ni wodi ya watoto ambalo limekuwa likiandikiwa fedha kila mwaka na haliishi na kufanywa ghara la kuhifadhi vifaa vya ujenzi ,dali zinadondoka zenyewe licha ya jengo hilo kuwa jipya ,jengo la mionzi kuwa na ufa korido karibu zote zina ufa .

Aidha Spika amesema kuwa changamoto nyingine ni mwili kukaa mwezi mzima sijui sababu ni nini,taarifa niliyopewa ni kweli hivyo polisi wapewe taarifa haraka .

Amesema baada ya kutoka hapo watafatilia polisi suala hilo ili liweze kufanyiwa kazi haraka maana kama mtu alichomwa moto lazima hali ya hewa ibadilike kwenye cjhumba cha kuhifadhia maiti .

Akitolea ufafanuzi wa malalamiko hayo ya wananchi yaliyotumwa kwa Dkt. Tulia kwa njia simu Mganga mfawidhi hospitali ya halmashauri ya Jiji la Mbeya , Dkt. Jonas Lundala amsema kuwa kweli wodi ya watoto haijaisha lilitumika kama ghara wakati tunafanya ujenzi wa majengo makubwa saba mapya wakati wanamalizia ujenzi lakini na sasa wanamalizia ujenzi wa wodi ya watoto mwaka wa fedha na kwamba mwaka wa fedha ujao mipango inawekwa ili kuweza kutenga fedha katika kumalizia jengo hilo.

“Mh. Spika kuhusiana na nyufa zilizopo zipo ambazio huwa zinatokea katika ujenzi wowote ambazo ni za kawaida ila sijapata taarifa ambayo ni hatarishi kuhusu nyufa kwenye majengo yao,kuhusu jengo la mionzi kudondoka ni kweli ,ila mh Spika naomba mhandisi anisaidie kujibu hili maana ndiye mtalaam”amesema Dkt. Lulandala.

Hata hivyo Dkt.Tulia amesema kuwa Mhandisi atafika kesho hapa hospitalini hapo kuangalia changamoto za majengo haya kwanini dali zinadondoka zenyewe licha ya kuwa majengo kuwa mapya na hayana muda mrefu toka yamejengwa .

Akijibu malalamiko mengine ya mwili kukaa kwa muda wa mwezi mmoja , Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igawilo ,Dkt. Grace Dugo amesema kuwa ni kweli kuna mwili umekaa kwa muda wa mwezi mmoja mwili huo uliletwa na polisi Uyole ambao walikuwa ulinzi wa siku huyo mtu hafahamiki alikutwa anaiba akapigwa na kuuwawa alikutwa akiiba pikipiki .

“ Sasa miili kama hii haturuhusiwi kuizika mpaka tupate taratibu za polisi zinasemaje ndo maana mwili huu upo mpaka sasa tukisubiri taratibu za polisi kwanza na mtu huyu hafahamiki “amesema mganga mfawidhi.

Akisoma ujumbe mwingine Dkt. Tulia amesema changamoto nyingine ni kutokuwa na Mganga wa mionzi kwa wanawake wajawazito hali inayofanya wanawake kutopata huduma kutokana na mganga kuwa likizo .

Akijibu swali hilo kutoka Spika wa Bunge Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Igawilo ,Dkt. Grace Dugo alisema kuwa ni kweli yupo likizo ila katika watalaam wa mionzi katika vituo vya Jiji wapo wawili tu kwa hiyo anapangiwa ratiba kwa yule ambaye yupo kituo cha afya Ruanda kwasasa anapangiwa ratiba ya kufika hospitalini hapo kwani amebaki peke yake.

Aidha Dkt. Tulia amesema changamoto hospitali ya wilaya kutokuwa na mtalaam wa mionzi inaleta maswali kidogo lifanyieni kazi kwa watalaam walifanyie kazi ,lingine ni viti mwendo vilivyotolewa kutotumika na leo alipofika mbunge kutolewa nje .

Mmoja wa wananchi wa Kata ya Igawilo ,Saida Hussein amesema yaliyosemwa ni kweli wanashukuru ujio wa Mbunge na yapo mengi hayo yaliyosemwa ni machache ila tunashukuru kumfikia mbunge .

Mwananchi mwingine, Rebeka Mwalongo amesema ni kweli kwenye hospitali hiyo kuna kero nyingi kwanini daktari apewe likizo wakati wanajua hakuna mtalaam katika hospitali ,mbunge awawasitize sababu wananchi wanateseka na changamoto za hospitali hiyo .