November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTB yaandaa onesho la SITE Dar

Na Bakari Lulela,Timesmajira

BODI ya utalii nchini (TTB) limeandaa onyesho maalumu la nane la Swahili international Tourism Expo (SITE), 2024 linalotegemea kuanza Oktoba 11 hadi 13  katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii Ephraim Mafuru amesema onyesho la site mwaka 2024 Lengo lake ni kuwakutanisha watoa huduma mbalimbali wa utalii.

“Onesho la SITE (Swahili International Tourism Expo) litawakutanisha wadau wa sekta ya utalii kutoka maeneo mbalimbali waliopo katika mnyororo wa thamani ndani na nje ya nchi,” amesema Mafuru 

Aidha Mafuru amesema kuwa tangu kuanzisha kwake Onyesho la Site limeendelea kuimarisha mtandao wa kibiashara hususan baina ya wafanyabiashara za utalii waliopo nchini na wenzao kutoka katika masoko ya utalii, hivyo kuchagiza ongezeko la watalii na sekta ya utalii.

Ameendelea kueleza kuwa Onyesho la SITE limekuwa likitoa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji ambapo mwaka huu linaongoza kwa kauli mbiu ‘Tembelea Tanzania kwa uwekezaji endelevu na utalii usiomithirika’.

Hata hivyo mkuu huyo alitaja nyenzo zitakazo ongoza SITE 2024 ni pamoja na sera ya Taifa ya utalii mwaka 1999, mkakati wa kutangaza utalii kimataifa (2020- 2025), mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano lll(FYDP III2021/22-2025/26),Ilani ya chama cha Mapindizi mwaka2025  na programu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Washiriki  SITE wanatarajia kushiriki ni zaidi  ya120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za utalii 120 kutoka nchi ambazo ni masoko ya kimkakati ya utalii wetu ikiwemo nchi za Asia, Ulaya na Amerika.

Mkuu huyo ameeleza wanatarajia kushiriki Onyesho la SITE ni pamoja na wakala wa biashara za utalii, watoa huduma za malazi, wakala wa safari, wakala wa meli za watalii, waongoza watalii, vyama vya utalii, wajasiriamali wa bidhaa za utalii,bodi ya utalii, Taasisi za uhifadhi, Taasisi za kifedha na Taasisi elimu za utalii.Kwa upande wa nchi zilizothibitisha kushiriki Hadi sasa ni China, Denmark, Finland, Japan, Afrika kusaini ,Hispania , India , Oman , Urusi ,Misri , Uholanzi , Nigeria, Brazil,Ujerumani , Kenya , Ethiopia , Uganda ,Lesotho na Tanzania.

Shughuli zitakazofanika wakati wa SITE ni maonyesho ya utalii, mikutano ya kibiashara,semina za masuala ya utalii na masoko, Jukwaa la uwekezaji katika sekta ya utalii, ziara za mafunzo za kutembelea vivutio vya utalii Wadhamini wa SITE kwa mwaka huu ni Air Tanzania , White sands hotel, Hanspaul, Sun Tours , Serena hotel, Onomo hotel, Urban hotel, ASAS , Brooklyn media , Peacock hotel na Kingiada hotelÂ