January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TSB:Wananchi changamkieni fursa ya zao la mkonge

Picha zote zinaonesha bidhaa ambazo zimetengenezwa kwa kutumia zao la mkonge

MKUU wa Sehemu ya Masoko na Uhamasishaji wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) David Maghali amesema zao la mkonge lina fursa nyingi ikiwemo katika utengenezaji wa gypsum na mapambo majumbani na maeneo mbalimbali.

Aidha ameziasa halmashauri kuratibu na kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi kulima zao la mkonge

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) yanayoendelea jijini Dodoma amesema,wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo kwa kulima zao la mkonge kwani maeneo ya kulima na masoko ni mengi.

Amesema kwa sasa wateja wa zao hilo ni nchi za Afrika Magharibi kama Nigeria,,Ghana,Morocco,Saud Arabia na Misri ambao hutumia katika kutengeneza bidhaa za ujenzi kama gypsum na mapambambo huku akisema Tanzania ndiyo imeanza kutumia teknolojia hiyo .

“Sekta ya mkonge ina fursa nyingi ambazo watu wanaweza kujiunga nazo,fursa namba moja ni wakulima kujiunga na kilimo cha mkonge ,mahitaji ya mkonge bado nni makubwa sana duniani lakiniuzalishaji wake bado ni mdogo,

“Kwa kuwa sisi watanzania bado tuna maeneo ambayo hayatumiki kwa chochote wala hayana uzalishaji,tunawahimiza serikali kupitia Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha mkonge ili kuinua wananchi wao kiuchumi lakini pia Bodi ya mkonge inaratibu masuala mbalimbali yahusuyo mkonge ,

“Kwa hiyo kwetu sisi mkonge siyo tatizo bali tunahitaji uratibu wa maeneo ya watanzania kufanya kilimo hiki,uwezo wa kufanya upatikanaji wa mashine kwa wakulima katika maeneo mwisho wa siku tutakuja kuratibu upatikanaji wa masoko aua uuzaji wa mkonge utakaokuwa umezalishwa.”amesema Maghali

Aidha amesema zao hilo lina bei nzuri huku akosema kwa saaa tani moja ya mkonge inauzwa kwa shilingi milioni 3.9 wakati miaka mitano iliyopita iliuzwa kwa shilingi milioni 2.5

Amewahakikishia wakulima kuwa,zao hilo lina uhakika wa kuvuna na kuuza.