Na Joyce Kaiki,Timesmajira,Mbeya
MENEJA wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Mbeya Musibu Shabani amewataka wananchi wanaoingia katika maonyesho ya Kimataifa ya Wakulima -Nane Nane kuhakikisha wanadai risiti kila wanaponunua bidhaa ili Taifa liweze kuingiza mapato kwa ajili ya ujenzi wa shughuli za maendeleo.
Akizungumza na waandihsi wa habari kuhusu ushiriki wa Mamlaka hiyo kweny maonyesho ya wakulima ,Shabani amesema,na wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwenye maoyesho hayo wahakikishe wanatoa risiti kila bidhaa wanayomuuzia mteja.
“Hii ni kwa mujibu wa sheria na kuepuka kuvutana vutana ,lakini pia wewe mfanyabiashara ukitoa risiti unaichangia nchi yako.”amesema Shabani
Aidha amesema TRA wapo katika maonyesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kutokana na mabadiliko mbalimbali ya sheria ya kodi yaliyopitishwa Bungeni hivi karibuni lakini kutatua changamoto za kikodi zinazowakabili wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Kodi Mwandamizi mkoa wa Mbeya Nicodemas Massawe amewasihi wakulima wa kati,wadogo na wakubwa watembelee banda hilo ili wajue ni bidhaa katika kilimo vimesamehewa kodi na vipi havijasamehewa na gharama zilizosamehewa ni kiasi gani ili iwe rahisi kwake hata kuagiza zana za kilimo ili mwisho wa siku kilimo kimletee tija.
Amesema,TRA ipo misamaha ya kodi iliyolenga sekta ya kilimo ili kusaidia kukua kwa kilimo kwa watu wengi zaidi kuagiza zana za kilimo kama vile matrekta na zana nyingine.
“Tunajua kabisa kilimo ndiyo utu wa mgongo wa Taifa na ndiyo chanzo cha chakula,kwa matrekta yakiingia yana msamaha wa kodi lakini pia tuna nyumba za kuhifadhia mazao ,mbolea na pembejeo nyingine zinazohusiana na kilimo vyote vina msamaha wa kodi .”amesema Massawe
Aidha amesema kwenye sheria ya kodi ya mapato ,mkulima anaweza akawa amegawanyika kwenye sehemu mbili,yupo anayelima kibiashara na anayelima kwa ajili ya chakula nyumbani na familia yake ambaye ni mkulima wa kujikimu.
“Sasa sheria yetu ya kodi ya mapato imewaweka katika makundi mawili namna gani sasa wanatakiwa kulipa kodi,kwa hiyo hapa mkulima anayelima kibiashara anatakiwa kulipa kodi ya mapato ili mradi mazao yake yafikie kiasi cha shilingi milioni 4 na chini ya hapo atakuwa ni mkulima anayelima mazao ya kujikimu na hatalipa kodi.”amesisitiza Massawe
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito