Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa mwaka huu wa fedha inatarajia kukusanya mapato ya kiasi cha tirioni 1.7 kutoka kundi la walipakodi wa kati 1692 huku ikiwataka wafanyabiasha kuendelea kutoa risiti za kieletroniki(EFD) kila wanapouza bidhaa.
Hayo yamebainishwa na Kamishina wa Kodi za Ndani wa TRA Alfred Mregi wakati wa uzunduzi wa Kitengo cha walipakodi wa Kati uliofanyika Novemba 6,2023 jijini Dar-es-Salaam ambapo ameeleza kuwa wanaimani kwa weledi walionao kundi hilo na hudu ambayo wamepanga kuitoa kama mamlaka watapita kiasi hicho walicho lenga.
“Kwa mwaka huu wa fedha matarajio yetu kwa kundi hili la walipakodi wa kati litatuzawadia kiasi cha makusanyo ya tirioni 1.7,”amesema Mregi.
Akizungumzia kuhusu kitengo cha walipakodi wa kati amesema kuwa kimeundwa na walipa kodi wa kati 1692 ambayo ni matokeo ya mabadiliko ya muundo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na inasimamiwa na Kamishina wa Kodi za Ndani kwa kusaidiana na Naibu Kamishina wa Divisheni hiyo .
Ambapo amesema kuwa wanaamini kuwa hatua hiyo itaboresha kwa kiasi kikubwa huduma zao na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwani ukusanyaji wa kodi ni wajibu wa kisheria.
“Kwa msingi huo ni wito wetu kwamba mkaendelee kutekeleza majukumu yenu ya ulipaji wa kodi kwa kuzingatia matakwa ya sheria kwani kufanya hivyo kunaweza kuwapunguzia gharama za uendeshaji wa biashara zenu pia kimsingi itakuwa imewezesha serikali kutoa huduma kwa jamii,”alisema Mregi.
Kwa upande wake Kamishina Mkuu wa TRA Alphayo Kidata aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wafanyabiashra wote nchini kuendelea kutoa risiti za kieletroniki(EFD) kila wanapo uza bidhaa.
Huku katika mauzo yao yote wahakikishe makusanyo na thamani ya fedha inayoandikwa iwe sahihi ili malipo katika mrejeo wa kodi(return) yanakuwa sahihi sambamba na kuwasisitiza wananchi waendeleze utamaduni wa kudai risiti za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.
Kidata amesema kuwa Julai Mosi mwaka huu TRA ilirasimisha rasmi muundo mpya wa utendaji kazi baada ya kupata idhini kutoka kwa Rais Samia na sasa mamlaka hiyo ina idara 13 ambapo idara mbili zinashughulika na makusanyo ya kodi ya mapato ya ndani ambazo ni idara ya walipa kodi wakubwa na kodi za ndani.
Ameeleza kuwa majukumu ya idara ya walipa kodi za ndani yametengwa katika vitengo viwili ambavyo ni kitengo cha walipa kodi wa kati na walipa kodi wadogo,lengo ni kuboresha utoaji wa huduma zao.
Lakini pia kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wateja wao ambao ndio msingi wa kuimarisha kazi zao huku wakitarajia kuongeza ufanisi katika uendaji kazi wao.
Pia ameeleza kuwa katika kuunda kitengo cha walipakodi wa kati TRA imejiwekea vigezo mbalimbali ambapo moja ya sifa muhimu ni kuwa mlipaji wa kodi kuanzia milioni 250 mpaka bilioni 2.5 kwa mwaka.
“Kigezo kingine ni ulipaji kodi wa hiari na kwa wakati kwa kuzingatia vigezo hivyo kitengo hicho kinawalipa kodi 1692 na wote wanatoka katika kanda zote,”alisema Kidata.
Aidha amesema kuwa wana kitengo kidogo ndani ya idara hiyo kinachoshughulika na biashara zinazofanyika mitandaoni ambapo kitengo hicho kina lengo la kukusanya kiasi cha tirioni 1.72,ikiwa ni asilimi 39 ya lengo ya idara ya kodi za ndani.
Hata hivyo ameeleza kuwa dhamira ya Rais ni msisitizo wake ambao amekuwa akiulekeza TRA kuwa ni vizuri wakawafanya wafanyabiashara na wafanyakazi wa mamlaka hiyo wasitumie shuruti katika kulipa kodi hivyo mamlaka imejikita katika kuimarisha mifumo na kuboresha mazingira ya wafany biashara.
Katika kutekeleza hayo kikamilifu mamlaka imeendelea kuimarisha mifumo ya kieletroniki ya kuwasilisha na kuboresha huduma kwa walipa kodi hivyo basi wanaendelea kuwaondolea usumbufu wa kuhitaji kuonana nao mara kwa mara.
“Mifumo tunayoijenga inamuwezesha mteja wetu kulipa kodi kwa wakati kwa namna hiyo uchochea ulipaji wa kodi kwa hiari na faida kubwa ya muundo huu mpya ni kuwasogezea huduma kwa ukaribu wateja wetu kila mlipa kodi atapata huduma bila usumbufu,”.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa uzinduzi wa kitengo cha walipa kodi wa kati.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza