January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRA watoa elimu ya mlango kwa mlango shinyanga

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Timu ya maofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wamefunga kambi katika mkoa wa Shinyanga lengo likiwa ni kutoa Elimu ya mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa mkoani hapo mjini pamoja na vijijini.

Zoezi hilo linaenda sambamba na ukusanyaji wa maoni na changamoto na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao kwa lengo kwenda kuyafanyia kazi kwa lengo la kuboresha zaidi na hatimae kurahisisha ulipaji kodi kwa hiyari.

Miongoni mwa changamoto zilizoripotiwa ni pamoja na umbali wa upatikani wa huduma, ambapo wafanyabiashara wanapotaka huduma za TRA wanalazimika kusafiri kwa masafa marefu kufuata huduma hiyo jambo linalowangezea gharama wanazotumia katika usfari na muda mwingi.

Aidha, baadhi ya wafanyabiashara wamefurahishwa na zoezi hilo ambalo limewasaidia kufamahu mambo mbali mbali ya kodi na kushauri zoezi hilo liwe endelevu ili waendelee kujifunza zaidi.