November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRA Mkoani Kilimanjaro walia na magendo

Na Martha Fatael, TimesMajira Online, Moshi

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA), mkoani Kilimanjaro, imeeleza kukerwa kwake na biashara ya magendo kupitia njia za panya katika wilaya za Rombo na Mwanga mkoani hapa.

Aidha TRA imeiangukia serikali mkoani Kilimanjaro kutaka juhudi za haraka na makusudi kukomesha biashara hiyo ambayo huathiri ukusanyaji wa Kodi.

Meneja wa TRA mkoani hapa Masawa Masatu amemweleza hayo mkuu wa Mkoa huo Nurdin Babu wakati wa maadhimisho ya wiki ya shukran kwa mlipa kodi.

“Niombe ofisi yako iingilie kati suala la magendo kwani imekuwa ni changamoto kwa Mamlaka katika ukusanyaji wa Kodi…mbali.na Hilo lakini tunaomba uhimize matumizi ya mashine za kieletroniki EFD” amesema.

Kadhalika Meneja huyo alielezea uwepo wa stempu za kieletroniki za bandia na hivyo kuikosesha TRA mapato.

Amesema pamoja na kuikosesha TRA mapato lakini pia Kuna uwezekano wa bidhaa zisizo na ubora sijapata stempu hizo na hivyo kuwaadhiri walaji.

Mapema Mkuu wa mkoa huo Nurdin Babu amesema serikali itazitaifisha bidhaa za magendo pamoja na magari yatakayotumika kubeba bidhaa hizo.

Amesema hatua hiyo Unalenga kukomesha biashara hiyo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa kiuchumi wa mkoa wa Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Babu ameipongeza TRA kwa kuvuka lengo la kukusanya Bil 227 Kwa mwaka 2021/2022 kati ya lengo la kukusanya Bil 210 kwa kipindi hicho.