November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPDC kuanzisha vituo vya gesi asilia Mikoa mitatu zaidi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MKUU wa Kitengo cha uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Marie Msellemu amesema , katika mwaka huu wa fedha ,Shirika hilo limepanga kuanzisha vituo vya gesi asilia mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma.

Muaellemu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandiahi wa habari kwenye vmaoneaho ya wakukima na wafugaji yanayoendelea katika viwanja vya 88 jijini Dodoma.

Amesema hatua hiyo itasaidia mtu kusafiri
kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia gesi asilia badala ya mafuta kwasababu ni rafiki kwa mazingira huku akisema hatua hiyo itasaidia watu wengi zaidi kuendelea kubadilisha mifumo ya magari yao kutoka kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye gesi.

“Vituo hivyo vitasaidia mtu kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Dodoma kwa usafiri unaotumia gesi asilia. Usafiri huu ni mzuri na salama kwasababu hautumii gharama kubwa na ni rafiki kwa mazingira,”alisema

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda aliipongeza serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Amesema serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga vituo vya kujazia gesi asilia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo Kwa wananchi.

“Serikali ya Awamu ya Sita inastahili pongezi kwa kuendelea kuweka Nguvu kubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na Sasa serikali inaendelea kujenga vituo vya kujazia gesi hiyo ili kuwahakikisha wale wote waliobadilisha mfumo kutoka katika matumizi ya mafuta kuwa huduma hiyo ipo,”amesema Msellemu