December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TotalEnergies yaendelea kufanyia maboresho vituo vyake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

KAMPUNI ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited imeendelea kuvifanyia maboresho vituo vyake vya mafuta kuwa vituo vya One Stop Shop.

Hiyo inatoa fursa kwa wateja wa kampuni hiyo wanapoenda kujaza mafuta kwenye kituo cha TotalEnergies anapata fursa ya kupata huduma zingine kwani kina duka la Café Bonjou ambalo linauza mahitaji mbalimbali ya nyumbani.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa kushirikiana na Royal Oven Bakery imefungua matawi la Royal Oven food concept katika baadhi ya vituo vyake kwa kuanzia na Kituo cha TotalEnergies kilichopo Barabara ya Bagamoyo eneo la Morocco ambacho kinatoa huduma za chakula, “fast food” .

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Jean Francois Schoepp alisema.

“Wateja ndio chachu ya biashara yetu na chachu ya mabadiliko, ukuaji na ubunifu wetu ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kukidhi na kuvuka mahitaji na matarajio yao kwenye huduma za TotalEnergies. Wiki hii tunawaalika wateja wetu, kufurahia huduma bora kutoka kwa maofisa wa TotalEnergies, kufahamu matangazo mbalimbali yatakayoendeshwa katika vituo vyetu na kushiriki nasi maoni kuhusu bidhaa na huduma zetu.” Alisema

Aliongeza kuwa kuwa; “Katika TotalEnergies tunaamini kuwa Wiki ya Huduma kwa Wateja ni zaidi ya kusherehekea wateja lakini pia kuwa na ubadilishanaji wa maana na kupokea maoni.Kwa hili tunawahimiza wateja wetu kutumia mifumo yetu ya mtandaoni ambayo itawasilishwa katika vituo wiki hii na kututumia maoni ambayo tutafurahi kuyapitia yote na kuboresha bidhaa na huduma zetu kwa kuridhika kwako.”

Alisema wanawakaribisha wateja wao kufurahia ofa na promosheni mbalimbali zinazopatikana katika vituo vyo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi.

Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano, Getrude Mpangile, aliwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye vituo vya vituo vya TotalEnergies katika katika mwezi huu wa huduma kwa wateja, na kusisitiza huduma kama hizi zinatolewa kwa mwaka mzima ambapo kwenye vituo vya TotalEnergies, sio tu utajaza mafuta bora na vilainishi vya hali ya juu vilioongezwa kiambata cha execillium, bali sasa utapata pia bidhaa mbalimbali za matumizi ya kawaida zenye ubora wa hali ya juu.

Wakati huo huo, Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited leo imehitimisha mwezi wa Huduma kwa Wateja katika kituo cha mafuta cha TotalEnergies Bagamoyo Rd, Morocco, yenye kaulimbiu ya “Pamoja kila hatua”

Menejiment na Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies kwenye picha ya pamoja kuhitimisha mwezi wa huduma kwa wateja, katika kituo cha mafuta cha TotalEnergies Bagamoyo Rd, eneo la Morocco.