Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania – TMX Godfrey Marekano ameeleza kuwa maandalizi ya uuzaji na uunuzi wa Korosho msimu 2024/25 yameanza na yanaendelea vizuri.
Marekano amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Agosti 13,2024 , huku akiwataka wakulima wa Korosho kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora ili kuziongezea thamani Sokoni.
“Tumekuwa na simu mzuri katika mazao mengine kama Kahawa,Ufuta, Cocoa na sasa Mbaazi, lakini wakati huohuo tumeshaanza maandalizi kwa ajili ya uuzaji wa Korosho kwa mfumo wa kielektroniki, naweza kusema maandalizi yanaenda vizuri ” amesema Marekano.
Kuhusu utaunzaji wa Korosho ghafi, amewashauri wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora pale watakapoanza mavuno ili kuendelea kuwavutia wanunuzi.
“kama nilivyoeleza kwenye mazao mengine, hata kwenye Korosho ni hivyohivyo, Wakulima waache udanganyifu,wasichanganye Korosho na uchafu mwingine usiofaa, wanunuzi wanafuatilia na wanazingatia sana ubora ili fedha wanayotoa iendane sambamba na thamani ya kile walichonunua” amesisitiza Marekano.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa