Na. Penina Malundo, Timesmajira
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Dkt.Adam Fimbo amewataka Waratibu wa Ufuatiliaji Usalama wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi wameshauriwa kutoa taarifa za matukio na madhara ya vifaa tiba na vitendanishi ili taarifa hizo zifanyiwe kazi na kutolewa mrejesho.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Udhibiti na Vfaa Tiba na Vitendanishi, Bryceson Kibassa ambaye alisoma risala kwa niaba ya Mkurugenzi TMDA wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TMDA kwa kushirikisha waratibu kutoka mikoa miwili ya Dar es Salaam na Pwani.
Amesema kuwa hayo ni mafunzo ya kwanza kufanyika kwa waratibu hao ambapo ni kuwajengea uelewa na uwezo katika eneo la ufuatiliaji usalama wa vifaa tiba na vitendanishi.
“Nyinyi ndio mmekuwa mkipokea na kukusanya taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi na kuwapatia nyenzo za kufanyia kazi ili taarifa zinazowasilishwa TMDA ziwe zimekamilika na kufanyiwa tathmini.
“Hivyo katika mafunzo haya mtajifunza juu a udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi kwa ujumla.
Hususani mtafundishwa jinsi na njia mbalimbali zitumikazazo na TMDA katika kufuatilia usalama yakiwemo matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizi na kuyatolea ufafanuzi” amesema.
Ameongeza kuwa, jukumu la udhibiti wa vifaa tiba lilikabidhiwa rasmi kwa iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2008 na udhibiti wa vitendanishi mwaka 2017 hivyo udhibiti wa bidhaa hizi haukuanza zamani sana kama ilivyo kwenye upande wa dawa.
Amesema kuwa pamoja na majukumu mengine ni kufuatilia taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa na vitendanishi lengo ni kufanya ufuatiliaji huu ni kutumiza dhima ya TMDA ya kulinda afya ya jamii kwa kuwakinga wagonjwa na watumiaji wasipate athari zinazotokana na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi vibovu.
Amesema pamoja na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha jamii na kufanya uhamasishaji kwa watoa huduma za afya, taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi zinazopokelewa ni chache sana.
“Kumekuwa na ongezeko la utoaji taarifa mpaka 254 lakini taarifa hizi ni chache ukilinganisha na idadi na wingi wa matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini” ameongeza.
Amesema kuwa kutokana na mafunzo hayo anaamini kutakuwa na ongezeko la utoaji taarfa za matukio na madhara ya vifaa tiba na vitendanishi hivyo ni vyema kutumia vizuri fursa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa lengo la TMDA ni luongeza upatikanaji wa taarofa hizi ili hatua za kiudhibiti ziweze kuchukuliwa na vfaa toba na vtendanishi visivyofaa na vyenye madhara viondolewe katika soko.
Naye Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adonis Bitegeko amesema kuwa ili kutambua kuwepo kwa vifaa tia visivyokidhi viwango hivi sasa kwa kila kituo cha kutoa huduma kuna fomu za rangi ya chungwa ambazo hutumika kutoa taarifa pindi mgonjwa anapohudumiwa na kupata changamoto kutokana na matumizi ya vifaa tiba ama dawa.
“Utoaji wa taarifa za wagonjwa ama watumishi kupata changamoto ya matumizi ya vifaa tiba visivyokidhi viwango ni mdogo hivyo kupitia karatasi hiyo ambayo mgonjwa atajaza pindi atakapopata changamoto iwe ya kushonwa na nyuzi kisha kukatika ama kutumia kifaa tiba chochote na kupata changamoto atatakiwa kujaza fomu hiyo au kutoa taarifa kupitia simu yake ya mkononi kwa kuingia kwenye ukurasa wetu mitandano ili na sisi tuweze kufanyiakazi changamoto hizo na kuzitolewa ufafanuzi” amesema.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam