Na Hadija Bagasha,TimesMajira Online, Tanga
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) imewatahadharisha wananchi kujiepusha na matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara ili kujiepusha na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ikiwemo kansa ya koo, kansa ya mapafu na kansa ya utumbo mpana.
Hatua hiyo imekuja baada ya tafiti kufanyika na kugundulika kuwa wamebaini kuwepo kwa magonjwa mbalimbali yatokanayo na matumizi ya tumbaku.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa mwandamizi elimu kwa Umma na huduma kwa wateja Roberta Feruzi wakati akizungumza na kituo hiki kwenye maonyesho ya 9 ya biashara na utalii yanayofanyika jijino Tanga.
Roberta amesema kuwa wao kama taasisi za mamlaka ya dawa na vifaa tiba ambao wamepewa dhamana ya kusimamia na kudhibiti bidhaa za tumbaku wametoa wito kwa wananchi kuacha kutumia bidhaa za tumbaku.
“Sisi TMDA kazi yetu kubwa ni kulinda afya ya jamii na kusimamia ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi lakini pia tuna majukumu makubwa ya kudhibiti bidhaa za tumbaku, “alisisitiza Roberta.
Aidha amesema TMDA wanatoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa lakini pia na matumizi sahihi ya vifaa tiba sambamba na vitendanishi.
Amesema watu wengi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya utoaji wa taarifa ya madhara ya dawa hivyo wapo kwajili ya kutoa elimu kwenye eneo hilo pindi mtu anapoona amepata maudhi madogo baada ya matumizi ya dawa.
“Eneo jingine ambalo hivi sasa mamlaka inasimamia kuanzia mwaka 2021 mwezi April TMDA ilikasimishwa matumizi rasmi ya kusimamia au udhibiti wa bidhaa za tumbaku pamoja na kwamba tuko kwenye maonyesho hapa Tanga lakini pia leo duniani ni siku ya kupinga matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara, “alisisitiza
Sambamba na hayo amesema wanaendelea kufanya usimamizi wa maeneo yanayofanya uuzaji na usambazaji wa bidhaa zote za tumbaku.
“Wito kwa wananchi inawezekana hawafahamu jambo hili TMDA inatoa wito kwa jamii kujiepusha na matumizi ya bidhaa za tumbaku lakini kingine kwa atakayepata elimu hii akawe balozi, “alisistiza Roberta.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba