Na Penina Malundo, timesmajira,Online
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam ambapo amefurahishwa na Mamlaka hiyo kushiriki maonesho hayo.
Akizungumza katika banda hilo,Waziri Ummy amesema amefurahishwa na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu ubora , usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa,vifaa tiba pamoja na vitendanishi pamoja na madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa za tumbaku.
Pia Waziri Ummy amesema TMDA inajipanga katika kuhakikisha masuala ya kutoa elimu hususani juu ya kemikali ambazo zipo katika bidhaa za tumbaku na katika kuelezea wamekuwa wakionesha kemikali za sumu ambazo zinapatikana kwenye tumbaku.
“Nimefurahi kuona Wananchi wanapata uelewa kwasababu suala zima la matumizi ya tumbaku linahitaji mtu awe na uelewa anapoingia katika matumizi yale ajue kabisa nini matokeo yake,”amesema
Akiwa katika banda hilo, maofisa wa TMDA wakiongozwa na Mkurugenzi wao Adam Fimbo wamemueleza Waziri kuwa wamekuwa wanahusisha wadau ambao wanamiliki maeneo ya wazi kuzingatia yale yanayotakiwa kufanyika kwa maana ya kutenga eneo maalum ya uvutaji lakini waweke alama za kuonesha uzuiaji wa matumizi ya kuvuta.
Waziri Ummy ambaye alikuwa ameambatana na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dk .Ted Chaiban ambapo naye ameonesha kufurahia hatua zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha umma kuhusu usalama na ubora wa dawa na vifaa tiba.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi