Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA) Kanda ya Magharibi imekamata dawa za binadamu zenye thamani ya sh mil 43 zilizokuwa zikiuzwa kinyemela kwenye maduka ya dawa kinyume na maelekezo ya serikali.
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Magharibi Kiboko Magigi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake.
Alisema dawa hizo zimekamatwa kutokana na msako mkali uliofanywa na Maafisa wa Mamlaka hiyo katika Mikoa 3 ya Kanda hiyo (Tabora , Katavi na Kigoma) ili kuondoa dawa zote zilizokatazwa na serikali katika maduka hayo.
Kiboko alifafanua kuwa kukamatwa kwa dawa hizo kunatokana na kukiukwa kwa kanuni ya 63 inayoelekeza aina ya dawa za binadamu zinazoweza kuuzwa katika maduka ya kawaida.
Alibainisha kuwa dawa zilizokamatwa ni zile zilizotolewa na serikali ili kusambazwa kwenye vituo maalumu vya watu wenye uhitaji ikiwemo Magereza na sio kuuzwa kwenye maduka binafsi.
Aliongeza kuwa dawa hizo baada ya kukamatwa dawa zimekabidhiwa kwa Jeshi la Magereza Mkoani hapa ili zitumike kuhudumia wafungwa waliopo katika gereza la Uyui.
Akipokea dawa hizo Kaimu Mkuu wa Gereza Kuu la Uyui Dkt.Richard Malifedha aliishukuru serikali kupitia TMDA Kanda ya Magharibi kwa kuwapatia dawa hizo ili kuboresha huduma za afya katika zahanati yao ya Gereza.
Alibainisha kuwa dawa hizo ni muhimu sana kwa wafungwa na makundi mengine ya kijamii kutokana na uhaba wa dawa uliopo ambao umekuwa ukiwakabili mara kwa mara .
Alisema Gereza hilo lina uhitaji mkubwa wa dawa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wafungwa waliomo .
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania