January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMA yatoa utabiri wa mvua maeneo yanayopata msimu mmoja kwa mwaka

Na Irene Clemence, TimesMajira Online

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kuanzia Novemba, mwaka huu hadi April, mwakani zitakazochagizwa na uwepo wa El-Nino.

Pia imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro, Iringa, Lindi, Mtwara, Singida naDodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema Leo Octoba 31 salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Ladislaus Chang’a amesema mvua hizo zinatarajiwa katika Kaskazini ya mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora na mvua za wastani hadi juu ya wastani kunyesha kusini mwa mkoa wa Katavi, Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma”amesema

‘Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya msimu wa Novemba, mwaka huu hadi Januari, mwakani kunatarajiwa kuwa na mvua nyingi ikilinganishwa na nusu ya pili ya Februari hadi April, mwakani”amesema

Pia amesama kutokana na mvua hizo shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama ilivyo kawaida katika maeneo mengi, hata hivyo vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinbu ya kilimo.

Aliendelea kueleza kuwa kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka hivyo aliwashauri wadau mbalimbali kuzingatia matumizi endelevu na uhifadhi wa rasilimali maji.

Amesema kuwa mfumo wa hali ya hewa unaonesha kuwepo kwa hali ya joto la bahari katika eneo la kati la kitropiki la bahari ya Pasifiki litakuwa juu ya wastani katika kipindi cha Novemba, mwaka huu hadi Aprili, mwakani.