Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu kimbunga Jobo kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari leo,imesema kumejitokeza mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga hafifu kwa jina Jobo.
Imesema Kimbunga hicho kipo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi na Mtwara.
Aidha, uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi hususani katika Pwani ya mwambao wa mikoa ya Mtwara na Lindi. “Mamlaka inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na kimbunga hicho ambayo inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa kimbunga Jobo katika wakati ujao,”imesema sehemu ya taarifa hiyo
Imesema Wananchi waendelee kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo