November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIRA yampongeza Rais Samia

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)imempogeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa kiwango cha akiba maalumu (fixed deposit)ili vijana waweze kujiajiri zaidi.

Akizungumza katika maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF),Meneja wa TIRA Frank Fred amesema lengo la kutoa kiwango hicho ni kutaka kuona sekta ya bima inakua zaidi na watu kutoa huduma kwa watu wengi na iliyo bora.

Amesema kiwango hicho kilikuwa ni changamoto kubwa kwa watoa huduma za bima kwa sababu gharama yake ni kubwa.

” Gharama ya kujiunga kuwa wakala wa bima ilikuwa ni sh.milioni 1.8 wameiondoa baada ya kusikiliza ushauri wa Serikali ikiwemo wadau wa sekta hiyo”amesema Fred

“Tunatekeleza agizo la Rais na tunamuunga mkono kwa juhudi anazozifanya katika kuendeleza ajira za vijana”aliongeza

Amesema hivi sasa wana makampuni wa wakala zaidi ya 32 ambapo kila kampuni kama itatoa ajira 100 kwa vijana kunakuwa na ajira 302 ambapo itapunguza tatizo la ajira .

Pia katika katika Maonesho hayo wamekuja kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya bima kuwa wameanzisha muongozo kwa makampuni ya simu kuweza kuingia ubia kwa wadau wa bima kwa kutumia simu za mkononi .

Aidha kupitia maonyesho hayo TIRA itatoa mafunzo kwa wadau wao ambao watakaopita katika banda lao kuhusu muongozo wa bima ya takafu ambayo itakayowawezesha watu wa dini zote kitumia muongozo huo.