December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIRA yawaasa wananchi kutumia bima Kwa manufaa yao.

Na David John Geita

MENEJA wa TIRA Kanda ya ziwa Richard Toyota Amesema kuwa Kwa ajili ya kuwapa elimu ya Bima wananchi hususani wa Kanda ya ziwa hivi Sasa wapo kwenye viwanja vya maonyesho vya EPZA Bombali mkoani Geita.

Amesema kuwa wamejipanga kutoa elimu kwa watanzania wote wakiwamo wachimbaji wadogo ,wakubwa na wawekezaji ,wakulima ,wafugaji,wavuvi na watu wa Kila aina ambao watakuwa wamefika kwenye viwanja hivyo.

Toyota ameyasema haya Septemba 26 mwaka huu kwenye viwanja hivyo vya maonyesho ya Teknolojia ya madini katika mahojiano yake na waandishi wa Habari waliotaka kujua ushiriki wao katika maonyesho hayo.

Meneja Toyota Amesema kuwa kwakuwa Bima ni ulinzi au Kinga Kwa mana hiyo Kila mtu anahitaji Ulinzi nakkwamba kwakuwa Kila mmoja anaasiliwa na majamba mbalimbali ya kiuchimi basi anahitaji kuwa na Bima .

Amefafanua kuwa jambo la msingi la kujiuliza ni kwamba wewe unahitaji Bima ya aina gani na kwamba misingi gani Kwa mafano wawekezaji wadogo wanabima za aina nyingi zinazomhusi Kulingana na shughuli zake anazozifanya.

” Mfano hapa mchimbaji anaweza kukabiliwa na majanga,janga linaweza kuwa ni ajali hivyo Kuna Bima ya ajali ambayo inamuhusu Yeye kumlinda Kwa masaa 24 akipata ajali basi Bima hiii inaweza kumlinda ,Bima ya afya , hii mtu mwenyewe anajikadilia kutokana na kazi yake ,hivyo likitoa janga au Yeye mwenyewe akifariki Kuna kuwa na fidia Kwa warithi wake kutokana na mchango wake “Amesema Meneja huyo

Amefafanua kuwa licha ya Bima hizo lakini Kuna Bima mbalimbali za biashara na kila mtu ambaye yupo hapo anaweza kukata Bima hiyo Kwa ajili ya biashara yake ila Kuna jambo lingine ambalo wanapaswa kufahamu hasa wananchi ambao wanafika kwenye maonyesho hayo na Kwa kutambua madhira ambayo wanayapa wakulima wameazisha Mpango mkakati wake.

Amesema kuwa Serikali wanakwenda kuweka fedha hapo kama ruzuku Kwa ajili yao na kumfanya mkulima kunufaika na Kwa upande wa makampuni yaliyoungana pamoja wanaenda kuweka Kinga kwenye mazao ambayo yamewekwa Kinga

Toyota Amesema kuwa Serikali inaweka fedha pale na kutokana na hilo itampunguzia mkulima kuingia gharama kubwa na kumrahishia Sasa kuingia kwenye soko la ushindani lakini vile vile na makampuni hayo yameungana pia kutengeneza kitu kinaitwa kosotie gesi ambapo lengo lake kubwa ni kwamba makampuni hayo yamekusanya mitaji yake na yameweka pamoja kwasababu miradi inayoendesha kwenye sekta ya madini na gesi ni mikubwa.

Amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo unaweka kinga kwenye masuala hayo hivyo makampuni hayo yanaungana pamoja na kuweka Kinga pamoja ya naleta utalaamu pamoja na kuweka Kinga pamoja Kwa ajili ya wale wafanya biashara mbalimbali, kwahiyo kupitia wawekezaji hao na wakija wakapitia kwenye kosotiani maana yake mitaji yao inakuwa Iko salama zaidi

Ameongeza kuwa pamoja na hilo TIRA kupitia maonyesho hayo wanawaambia watanzania Kuna watu wanatumia vyombo vya moto hivyo magari yote hayatakiwi kutembea barabarani pasipokuwa na Bima na ikiwa chombo hicho hakina Bima na wewe mwananchi umesafiri nacho manaake dhamana au reability ya kusafiri na hicho chombo lazima ilipwe na mmiliki.

Ameongeza kuwa kama chombo kina bima manaake dhamana inakuja kwenye kampuni ya Bima hivyo wananchi wanaeleweshwa kwamba Kuna mfumo ndani ya Bima umeazishwa wa kuhakiki usalama wa chombo alichopanda Kwa kutumia simu yake ya mkononi akiwa kama abiria .

Toyota Amesema kuwa kwakutumia simu Yako ya mkononi utabonyeza x152 x00# alafu utachagua namba 3 alafu namba 4 alafu namba 1 na mwisho utaingiza namba ya gari au chombo na itakuletea taarifa ya chombo hicho na lengo ni kufanya mtanzania huyo atakapokuwa amepatwa na tatizo apate haki ya kumwezesha kurudi kwenye shughuli zake.

Amesema kwasababu Kampuni ya Bima ikikufidia hata kama umepata ulemavu wa kudumu lakini angalau anaweza kujikimu na kuendelea familia yake hivyo ndio maana wapo Geita ili wananchi wapate elimu ya masuala ya Bima Kwa maana ni ulinzi wa maisha yao.