Na Mwandishi wetu
WIZARA ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na makundi maalumu imesema tayari imepeleka timu ya wataalamu wa ustawi wa jamii mkoani Manyara kwa ajili ya huduma ya msaada wa afya ya akili na kijamii kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliosababishwa na mvua katika mlima Hanang.
Hayo yamebainishwa Dar es salaam leo na Waziri wa wazara hiyo, Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya ustawi wa jamii na miaka 50 ya chuo Cha ustawi wa jamii .
Amesema kufikia Disemba 8 mwaka huu wataalamu hao wameishatoa huduma kwa watu 823 ambapo kati yao 440 ni wale waliopo katika kambi tatu za Katesh, Genambi na Ganana .
Amesema watu 327 ni wale waliopo katika jamii huku 56 ni wale waliokuwa hospitali .
“Nachukua fursa hii kuwapogeza sana wataalamu wetu wa ustawi wa jamii na Maendeleo jamii walioko huko katika eneo la tukio na ambao wameendelea kufanya kazi hizi usiku na mchana pasipo kuchoka …pia tunawaombea heri wale wote ambao bado wanaugua katika majeraha Mungu awasaidie wapone Kwa haraka na wote waliotagulia mbele ya Haki ,”amesema.
Aidha ameipongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa ustawi wa jamii na kuunda wizara hiyo mahususi inayosimamia ustawi na Maendeleo ya jamii .
“Serikali imekuwa ikitoa nafasi za ajira kwa wataalamu wa ustawi ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/24 amehaidi kuongeza nafasi za ajira 350 huku Serikali ikiendelea kuongeza maofisa hao ili kupanua wigo upatikanaji wa huduma za kiustawi nchini,”amesema.
Akizungumzia kuhusu Maadhimisho hayo Dkt Gwajima amesema maadhimisho hayo yalizinduliwa rasmi mkoani Dodoma Septemba 6 mwaka huu na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dotto Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Amesema baada ya uzinduzi huo kulifuatiwa na utoaji elimu na huduma za kiustawi katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Geita, Kigoma, Songwe.
Amesema kwasasa huduma hizo zitatolewa mkoani Dar es salaam bila malipo katika Viwanja vya mnazi mmoja kuanzia Disemba 14 hadi 17, mwaka huu huku kilele cha Maadhimisho hayo kitafanyika katika ukumbi wa mwalimu Julius Nyerere Disemba 18 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
“Lengo la Maadhimisho haya ya wiki ya ustawi wa jamii na miaka 50 ya chuo cha ustawi wa jamii ni kutagaza huduma za ustawi wa jamii na kuamasisha jamii kuweza kuzifikia kwa ukaribu huduma hizo sambamba na kusherekea miaka 50 ya utoaji huduma kwa chuo Cha ustawi wa jamii ambacho kimekuwa kikizalisha wataalamu wa ustawi wa jamii tokea mwaka 1975 ,”amesema.
Aidha katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaam maadhimisho hayo yataambana na huduma mbalimbali ustawi wa jamii zikiwemo usajili wa vituo vya kulelea watoto, huduma za kuasili watoto, huduma za malezi ya kambi Kwa wenye huitaji wa watoto wa kuwalea , usuluhishi wa migogoro ya ndoa , elimu ya masuala ya Haki na ustawi wa mtoto, afya ya akili na msaada wa kisaikolojia pamoja na elimu kuhusu huduma zinazotolewa na chuo cha ustawi wa jamii .
Vilevile ameseema kutakuwa na huduma za afya ambazo zitaambatana na vipimo mbalimbali ikiwemo macho, uchunguzi wa afya ya masikio, kisukari, elimu ya lishe na shinikizo la damu .
Ameongeza kuwa nyingine zitakazotolewa ni huduma kwa watu wenye ulemavu, huduma za utoaji wa vyeti vya kuzaliwa pamoja na elimu ya masuala ya ukatili na namna ya kukabilina na ukatili katika jamii .
Aidha ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika wiki ya ustawi wa jamii .
Kwa upande wake Kamshina msaindizi wa ustawi wa jamii, Baraka Makona amesema katika kuadhimisha maadhimisho hayo wanajivunia kuongeza wigo wa kukabilina na mazingira hatarishi kwa watoto ambapo wamekuwa wakiwauganisha na huduma mbalimbali.
“Tumeboresha huduma za malezi ya kuamimika Kwa watoto..sekta nzima imeboreshwa zaidi na chuo hiki ni Sehemu ya mafanikio”amesema Makona.
Mwisho
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano