December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo,Zmotion yawapa somo wamiliki wa shule binafsi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Tigo na ZMotion wametoa mafunzo ya mfumo wa malipo ya Ada kwa wamiliki wa shule binafsi Tanzania kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ ni mojawapo ya ubunifu wa kiteknolojia uliolenga kutatua changamoto zinazowakumba wazazi na shule katika suala la ulipaji ada.

Aidha, Malipo kwa kupitia mfumo huo yatakuwa yakifanyika kupitia huduma ya TigoPesa, hivyo kurahisisha mchakato mzima.

Mafunzo hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam, yakiwa na lengo la kuhakikisha ufanisi wa mfumo huo mpya ambao unatoa fursa kwa wazazi kulipia ada kidogo kidogo kulingana na uwezo wao ambapo mafunzo hayo yametolewa kwa siku moja kwa wamiliki na wakurugenzi wa shule binafsi kuhusu huduma yetu mpya ya LIPA ADA.

Naye, Mkurugenzi wa Biashara-Tigo Pesa, James Sumari, alieleza kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ ni mojawapo ya ubunifu wa kiteknolojia uliolenga kutatua changamoto zinazowakumba wazazi na shule katika suala la ulipaji ada.

Hivyo, Mkurugenzi wa ZMotion Said Ally amebainisha kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ umesanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya shule binafsi na ni rahisi kutumia