December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Karatu

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Kampuni ya Mawasiliano Tigo, imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wahanga/waathirika wa mafuriko Wilayani Karatu

Akizungumza wakati wa utoaji Msaada huo, Meneja mauzo wa Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya ametoa pole kwa wakazi wote wa Karatu lakini pia serikali kwa maafa yaliyowatokea wananchi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao.

“Leo Tigo tupo hapa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu kufuatia maafa ambayo walikumbana nayo ndugu zetu wa Karatu yaliyoathiri maisha ya watu na kukosa maeneo ya kuishi ambapo mpaka sasahivi wanahifadhiwa na ndugu na jamaa, hivyo Tigo kama sehemu ya jamii imeona ni vyema na sisi tushiriki tuwafariji wenzetu kwa chochote “

“Tunakabidhi vitu mbalimbali ambavyo vitaenda kuwasaidia wenzetu kwa muda ambao wamepatwa na tatizo hilo”

“Tumekabidhi magodoro, mablanketi, unga, mchele, maharage na maji ambavyo tunaamini ni vitu ambavyo vinatumiwa kilasiku na vitawasaidia ndugu zetu”

“Tigo tuko pamoja nao na tutaendelea kushirikiana nao kwa namna yoyote” Alisisitiza

Kwa upande wake Amina Mohamed, Muathirika wa mafuriko hayo, ameishukuru Tigo kwa msaada huo na kuiomba serikali iwasaidie kutoa maji hayo kwani bado wanahangaika hasa katika sehemu ya malazi.